KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab, akifungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa huduma za uchapaji na vifaa vya ofisini na kuandikia, ulioandaliwa na wakala wa uchapaji wa serikali Zanzibar huko Gombani Pemba
NA ABDI SULEIMAN.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, amewataka Maafisa wa dhamini na wakuu wa maidara wa taasisi za serikali, kuitumia idara ya uchapaji kwa kuchapisha kazi zao na ununuzi wa vifaa vya maofisini.
Aidha alisema serikali imeanzisha idara hiyo maalumu, ili taasisi za serikali kuweza kupeleka kazi zao kuchapiwa kwa kuepuka siri za serikali kuzitoa njee, pamoja na ununuzi wa vifaa vya maofisini.
Katibu Mkuu huyo aliyaeleza hayo, wakati wa Mkutano wa wadau wa huduma za Uchapaji na vifaa vya ofisini na kuandikia ambavyo vipo Gombani, mkutano uliofanyika Mjini Chake Chake.
Alifahamisha kuwa idara ya uchapaji ni sehemu salama, kwa kupeleka kazi zote za uchapaji za serikali, kuliko kupeleka kwenye taasisi za nje, kufanya hivyo ni kuzitoa nje siri za serikali.
“Sisi watendaji ni jukumu letu kuwasimamia maafisa wetu wa manunuzi, tuhakikishe mambo yote ya nayohusu manunuzi yananunuliwa katika idara yetu, tena hapa tunaweza kupeleka tenda na kuwapatia idadi ya vitu tunavyotumia kwa mwaka mzima na wakatuagizia”alisema.
Akizungumzia sual la Rushwa, alisema serikali ya awamu ya nane inapiga vita sana suala la rushwa, sisi kama watendaji wa serikali na wakuu wa maidara, tujitahidi sana kuwaongoza maafisa manunuzi wetu, ili kuepuka kutupeleka katika sehemu ambazo sizo.
“Taizo kubwa hata ni hii Ten pasent inayogombaniwa, hivi sasa serikali iko macho sana tuepuke matatizo ya rushwa, kunatatizo katika maduka kuwa na risiti za aina mbali mbali, hapa tunapaswa pia kua makini sana”alisema.
Akiwasilisha mada juu ya uanzishwaji na uwezo wa kisheria ZGP, Kaimu Mkurugenzi wa ZGP Salum Rashid Suwedi alisema taasisi za serikali ni lazima kupatiwa huduma zake za uchapaji na ununuzi wa vifaa kutoka ZGP na sio kwenye taasisi nyengine.
Alisema tayari wamejipanga kuhudumia taasisi na tayari Pemba wameshaleta vifaa vya bohari, huku akiwataka viongozi wa taasisi kuwa makini na maafisa wao manunuzi katika kununua vifaa.
“Mwisho wa siku taasisi zinajulikana ambazo zimenunua vifaa kutoka kwetu na ambavyo wahajanunua, ndio pale munapoona munawekewa kwiri nyingi katika suala la manunuzi kwa kutokununua vifaa katika ofisi yetu”alisema.
Hata hivyo aliwataka maafisa wadhamini na watendaji, kuwa makini na maafisa manunuzi wao, kwani baadhi ya maafisa manunuzi wanawapotosha mabosi wao katika suala zima la ununuzi wa vifaa vya ofisini.
Kwa upande wake Mkurugenzi uhusiano kwa umma, masoko na bohari kuu ZGP, Hannat Mohamed Aboud akiwasilisha mada ya huduma za bohari kuu ya vifaa vya ofisini na kuandikia na taratibu za upatikanaji wa huduma, alisema ili taasisi iweze kupata huduma vizuri kwa taasisi kulipi asilimia 50% malipo.
Naye Mdhamini wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Salum Ubwa, alisema maafisa manunuzi zaidi wanaangalia 10% kuliko kufuata sheria katika suala la manunuzi.
Alisema kuwepo kwa idara ya uchapaji na taasisi kupeleka kazi zake, zitasaidia urujeshaji wa fedha za serikali zinarudi serikalini na kutumika katika matumizi mengine.
Nao baadhi ya wawakilishi wa maafisa wadhamini, wameipongeza serikali kwa uletaji wa vifaa pamoja na kuwepo na idara ya uchapaji pemba, kwani wataweza kupunguza kutumia taasisi za njee kuchapisha.