Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amewasili katika uwanja wa ndege wa ABEID AMANI KARUME -PEMBA, kuendelea na ziara yake ya kichama katika mikoa minne ya kichama kisiwani pemba.
Akiwasili katika uwanja wa ndege Mheshimiwa Othman amepokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali,Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi pamoja na wanachama wa Chama cha ACT
Wazalendo