NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Wafanyabiashara kisiwani Pemba wamesema wao ni wadau wakubwa wa kulipa kodi hivyo ni vyema kodi hizo zikatumika kwa kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili.
Wafanyabiara hao wamesema hayo huko katika ukumbi wa Maktaba Chake Chake wakati walipokuwa wakichangia katika mafunzo ya kuwasilishaji wa ritani kwa njia ya mtandao.
Wamesema miungoni mwa matatizo yanayowakabili ni miundo mbinu ya bara bara kwani ni moja kati ya kichocheo kikubwa katika kuimarisha biashara zao pamoja na kuleta maendeleo nchini lakini bado kwao wao ni kikwazo.
Wakizungumzia juu ya mfumo wa uwasilishaji wa ritani kwa njia ya mtandao wamesema mfumo huo utawasaidia kurahisisha kufanya shughuli zao kwa wakati hivyo wameiyomba mamlaka ya mapato kutoa elimu ipasavyo ili waweze kufanya kazi hizo kwa ufanisi zaidi.
Nao maafisa kutoka mamlaka ya mapato Tanzania kwa upande wa Zanzibar wamesema watahakikisha wanatoa elimu hiyo ipasavyo ili walengwa waweze kuitumia kama ilivyokusudiwa.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI