Ungefikiria ni binadamu pekee ambaye angeweza kufanya safari yamwendo mrefu kutafuta mpenzi au hata mapenzi .Lakinio sio kwa sababu hata wanyama kumbe wanahitaji mapenzi pia.
Kifaru mweupe wa miaka mitano amesafiri kutoka Taiwan hadi Japani – yote hayo yakiwa ni sehemu ya kumtafuta mpenzi.
Kifaru huyo kwa jina Emma ameanza kuishi Japani katika hifadhi ya wanyama ya Tobu, pamoja na kifaru wa miaka 10, Moran.
Kifaru huyo alichaguliwa kati ya kundi la vifaru 23 watakaopelekwa Japani kwasababu ya haiba yake huku wafanyakazi wakisema kwamba “ni nadra sana kwake kuanza kupigana na wengine”.
Kupelekwa katika hifadhi ya wanyama ya Japani ni jaribio la kuongeza idadi ya vifaru weupe barani Asia.
Vifaru mweupe wanachukuliwa kuwa katika hatari ya kutoweka, kulingana na shirika la Hazina ya Ulimwengu ya Mambo ya Asili (WWF) ikiwa wamesalia 18,000 pekee.
Emma aliwasili Japani Jumanne baada ya kusafiri kwa karibu saa 16 kutoka mbunga ya wanyama ya Leofoo Safari huko Taiwan makazi yake ya asili.
“Baada ya kucheleweshwa kwa sababu ya janga la virusi vya corona, Emma, kifaru mweupe wa kusini, aliwasili katika hifadhi yetu Juni 8, jioni,” taarifa katika hifadhi ya Japani imesema.
“Tulifungua taratibu kontena iliyokuwa imetumika kumbeba ambayo iliwekwa mbele ya eneo lake la kulala. Emma, bila kuonesha dalili za aibu, alikwenda moja moja hadi chumba chake cha kulala,” iliongeza.
Awali, alikuwa amepangiwa kusafiri mnamo mwezi Machi, lakini kama mamilioni ya watu kote duniani, mipango hiyo ilicheleweshwa kutokana na virusi vya corona.
Hatahivyo, muda huo ulitumika kumuandaa vilivyo katika safari yake huku waliokuwa wakimtunza wakianza kumzungumzisha lugha ya Kijapani kama vile “njoo” na “hapana” ili aanze kuzoea.
Wafanyakazi wa hifadhi ya Leofoo Safari awali walikuwa wamesema kuwa udogo wa Emma ulifanya kusafirishwa kwake kuwa rahisi.
Hifadhi za wanyama zimekuwa na machango mkubwa katika kuongeza idadi ya vifaru weupe.
Hata hivyo wenzao wa kaskazini hawajakuwa na bahati ya kuishi ikiwa wamesalia wawili pekee. Wote wa kike, hilo likimaanisha kwamba spishi hiyo ina uwezekano mkubwa wa kupotea kabisa – na kutoa changamoto kwa wanasayansi kufatuta mpango makhususi wa kuwaokoa.
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Uwindaji haramu ni tishio kubwa la kwanza linalokabili spishi hiyo.
Soko haramu likiwa limeshamiri kwa pembe zake, ngozi na kucha ambazo zimetengenezwa kwa keratini inayotumika kama dawa ya kuongeza ashki (aphrodisiac) au tiba ya kansa ambayo bado haijathibitishwa kutumia utafiti wa kisayansi