Rais wa Marekani Joe Biden amewasili nchini Uingereza katika ziara yake ya kwanza rasmi Ulaya.
Ni kituo chake cha kwanza katika ziara ya siku nane huko Ulaya. Atahudhuria mkutano wa viongozi wa G7 mjini Cornwall na kukutana na Malkia kabla ya kuvuka na kuhudhuria shughuli zingine rasmi- ikiwa ni pamoja na kongamano lake la kwanza la Nato akiwa rais, na kumalizia ziara yake kwa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Geneva.
Safari ya Bw. Biden inajumuisha mambo mengi. Rais wa Marekani huandamana na usafiri maalum utakaomsaidia kutoka sehemu moja hadi nyingine, ardhini na angani.
Na hakuna cha kushangaza zaidi kuliko ndege ya rais ya – Air Force One.
Ndege hiyo ilitua RAF Mildenhall mjini Suffolk siku ya Jumatano, ambapo Bw. Biden alikutana na maafisa wa Marekani walioko hapo kabla ya kuelekea Cornwall.
Kama inavyoeleza tovuti ya White House , Air Force One ni ishara ya kudhibiti trafiki ya anga kwa ndege yoyote ya kikosi cha angani iliyombeba rais wa Marekani.
Lakini sehemu kubwa ya neno hilo linatumika kuashiria ndege mbili maarufu za rangi nyeupe na bluu – ndege maalum ya Boeing 747-200B – ambazo zina nambari 28000 na 29000 sehemu ya nyuma.
Ndege ya Air Force One imeundwa kwa njia ambayo ina uwezo wa kuzuia athari zozote za shambulizi zinazoweza kuharibu mifumo yake ya eletroniki kama vile kulipuliwa kwa bomu la nyuklia angani.
Ndege hiyo pia huwekewa vifaa vya mawasiliano ya kijeshi na vifaa vya kujikinga yenyewe.
Hii inamaanisha kuwa Air Force One ina uwezo ya kuzuia makombora.
Ndani yake ina nafasi ya futi 4,000 mraba ambayo imesambazwa kwa viwango vitatu. Kando na sehemu ya rais kulala, pia kuna kituo cha afya , seheumu ya kula, na sehemu ya washauri, Maafisa ulinzi wa Huduma ya Siri na waandishi wa habari.
Kwa safari fupi za angani, rais hutumia helicopta – inatambulika kutokana na rangi ya kijani kibichi na juu nyeupe.
Marine One – pia sio helikopta moja, bali ni jina lililopewa ndege kadhaa Jeshi la Majini ambazo humbeba rais wa Marekani – huwa zinajulikana kama VH-3D Sea King au VH-60N White Hawk.
Kuna ndege nyengine zinazofanana na Marine One ambazo huandamana na ndege hiyo ya helikopta. Ndege hizo mbili zinazojulikana kama Green Top hutumika kuisindikiza ndege ya rais.
Wasomaji wa Uingereza huenda wanakumbuka ndege aina ya tilt rotor iliokuwa angani wakati wa ziara ya rais Donald Trump mwaka 2018. Ndege hizo zinaweza kupaa wima na zinaweza kufanya kazi kama helikopta na vile vile ndege ya kivita.
Mara baada ya kutua, Rais Biden anatoka kwa Air Force One au Marine One na kuingia gari la aina ya Cadillac iliyopewa jina la utani la- The Beast.
Gari hilo lenye urefu wa mita 5.5 sawana (futi 18) linaweza kubeba watu watano na pia lina vifaa tofauti za matibabu, ikiwemo jokovu lenye damu inayoendana na aina ya damu ya rais, endapo kutatokea hali ya dharura.
Kizazi kipya cha the Beast kilianza kutumika mwaka 2018. Gari hilo liliundawa na kampuni ya General Motors na maafisa wa ujasusi hawakutoa maelezo zaidi kuhusu usalama wake. Lakini ripoti zinaashiria kwamba lina uzani wa tani tisa (20,000lb), mwili wake umeundwa kama gari la kivita na madirisha hayawezi kupenyeza risasi.
Inaripotiwa kuwa na vifaa vya kurusha vitoa machozi, kamera za kufanya kazi gizani na simu ya satellite.
Shina la gari hilo limejengwa na chuma kinachoweza kulilinda dhidi ya shambulio la bomu.
Matairi yake yanaweza kufanya kazi hata yakipata pancha au kutoboka
Hata hivyo mkondo wa ziara yake Cornwall, rais amaeamua kuachana na The Beast, na badala yake kutumia gari aina ya SUV.
CHANZO CHA PICHA,PA MEDIA
Maafisa wa kijasusi walikuwa tayari wamesafiri Cornwall kuchunguza eneo litakalofanyiwa mkutano wa G7 summit – kupanga njia atakazopitia hasa eneo hilo la vijijini.
Ziara ya Rais wa wa zamani Barack Obama kwenda Downing Street mwaka 2009 ilipata umaarufu baada ya gari lake kupata changamoto kugeuka katika barabara hiyo maarufu. Dereva alipoeenda safari nyingini mwaka 2016 alifanikiwa .
Eneo hilo limethibitiwa kabisa na linaweza tu kufikiwa kupitia Carbis Bay ambayo ni pwani ya kaskazini mwa Cornwall, ambako viongozi wa ulimwengu wamekusanyika.
Nchi saba zenye uchumi mkubwa zaidi duniani zinakutana katika kongamano la G7. Kandona Marekani, nchi zingine ni Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia na Canada. Muungano wa Ulaya pia unawakilishwa.