Thursday, January 9

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akihoutubia katika madhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani huku akimuagiza Waziri mwenye dhama wa Wizara ya Afya kuwaeka watendaji wenye uwezo na ubunifu katika kukiendeleza kituo cha damu salama
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Phillip Isdor Mpango akiwasili Zanzibar kwa mara ya kwanza tokea alipoteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN, akipitia katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Abeid Amani Karume huku akipokelewa na makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe. HEMED SULLEIMAN ABULLA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimkabidhi cheti maalum Askari Meja Mwamvura Silima Salum wa kikosi cha J.K.U kwa niaba ya kikosi hicho kwa kujitoa kwao katika zoezi la uchangiaji wa damu.
Waziri wa wa Afya ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazuri akiwahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha yaw engine katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya watendaji wa kitengo cha damu salama kilichopo Amani kwa Wazae Sebleni wakati akiwasili katika Ofisi hizo katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka Uongozi wa Wizara ya Afya kuongeza nguvu katika kitengo cha damu salama kwa kuwaongezea vitendea kazi watendaji wao pamoja na kujali  stahiki zao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Mhe. Hemed alieleza  hayo katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani, illiyofanyika katika Ofisi ya Benki ya uchangiaji damu Sebleni  wilaya ya Mjini Unguja.

Aliwapongeza wafanyakazi wa kitengo hicho kwa kazi kubwa wanayofanya katika kijitoa kwao kwa moyo mmoja kwa kuhakikisha wanafikia lengo la ukushanyaji wa damu kwa wingi ili kuoka maisha ya watu wkiwemo mama wajawazito, watoto na watu waliopatwa na ajali.

Alisema kuwa kutokana na suala la uchangiaji damu kumgusa kila kila mmoja katika jamii linahitaji kupewa kipaumbele bila ya kuangalia itikadi za kisiasa, kidini na kikabila.

Makamu wa Pili wa Rais alimuagiza Waziri wa Afya, ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto kuzingatia kuwaeka kwenye nafasi watu wenye uwezo watakaosaidia kuimarisha kitengo hicho cha damu salama.

Alifafanua kuwa, kumekuwepo kwa tabia isioridhisha kwa baadhi ya wakurugenzi katika wizara hiyo kuingilia utendaji kazi wa kitengo jambo ambalo halitoi tija na linawanyima uhuru watendaji waliopo katika kituo hicho.

Akigusia suala la ubuniufu Mhe. Hemed aliwataka watendaji wanaofanya kazi zao katika kituo hicho kuwa wabunifu katika kuongeza ufanisi wa kazi badala ya kutegemea bajeti kutoka serikalini.

Aidha, katika maadhimisho hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kwa ushirikiano wanaouonesha hasa wa kuanda mabonanza mbali mbali ya uchangiaj wa damu, akitolea mfano kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani , ambapo walisaidia kukusanya chupa 1650 na kusema kuwa huo ni ushirikiano unaotakiwa katika kupeleka mbele gurudumu la maendeleo Nchini.

“Nawapongeza sana wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwa mstari wa mbele katika uchangiaji wa damu jambo ambalo linatoa manufaa kwa wananchi” Alisema Makamu wa Pili

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed alitoa rai kwa wananchi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia damu na liwatoa  hofu kuwa suala la uchangiaji damu ni salama ambapo wafanyakazi wanaotoa huduma katika kitengo hicho wana utaalamu, uweledi na umakini wa kutosha katika kuhakikisha wanalinda afya ya wachangiaji kabla na baada ya kuchangia.

“Niwaombe sana mzidi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia damu kwa hiari ili tuwe na akiba ya kutosha kwa matumizi ya kila siku” Alisistiza Makamu wa Pili wa Rais

Nae, Waziri wa Afya ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazuri alitumia fursa hiyo kuwashajihisha watu kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha maisha watu.

Alieleza kwamba, uzoefu unaonesha uhitaji wa damu Zanzibar ni mkubwa Zaidi kuliko kiwango kinachochangiwa akitolea mfano kwa mwaka jana Uniti elfu Kumi na Sita zilikusanywa lakini uhitaji wa damu ulifikia kiwango cha Unit Elfu Ishirini na Saba.

Alisema kuna umuhimu wa watu kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwani Uniti moja ya mchangiaji ina uwezo wa kuoka maisha ya watu watatu jambo ambalo lina tija kubwa kwa jamii.

Siku ya uchangiaji damu kwa hapa zanzibar huazimishwa  kitaifa kila mwakaili kuungana na mataifa mendgine duniani kwa lengo la kuwasaidia wahitaji ambao wapo hatarini kupoteza maisha.

kauli mbiu ya mwaka huu inasema “DAMU NI UHAI CHANGIA DAMU MAISHA YAENDELEE”.

……………………………….

Kassim Abdi

Ofisi ya Mkamu wa Pili WA Rais wa Zanzibar.