Monday, November 25

Mgogoro wa Tigray-Ethiopia: Baa la njaa lililosababishwa na binadamu

“Sasa hivi Tigray kuna ukame.”, Mratibu wa masuala ya dharura wa Umoja wa mataifa Mark Lowcock, ameelezea kwa uwazi kabisa hali ilivyo huko kaskazini mwa Ethiopia, Alhamisi.

Katika taarifa yake – iliyotolewa wakati wa majadiliano ya mkutano wa G7 iliangazia tathmini ya mgogoro huo iliyotolewa na shirika la utoaji chakula la Umoja wa Mataifa.

Katika ripoti yake inakadiriwa kuwa watu 353,000 huko Tigray walikuwa katika awamu ya 5 ya janga hilo na milioni 1.769 zaidi zimetengwa katika awamu ya 4 ya mpango huo.

Hiyo ni namna tu ya kusema kwamba kuna “baa la njaa”. Ingawa shirika hilo halikutumia neno hilo kwasababu za kisiasa – ingawa serikali ya Ethiopia ingepinga hilo.

Pia nyuma ya idadi hiyo, kuna ukiukaji wa haki za binadamu uliotokea. Idadi kubwa ya vifo iliyotokana na ukosefu wa chakula haikuweza kuepukika. Tayari hilo limeshatokea.

Raia wa Tigray wanazungumzia watu waliopatikana wamefariki dunia katika maeneo ya vijijini asubuhi wakati watu wana amka.

Wanawake waliotekwa nyara na wanajeshi na watumwa wa ngono wapo hospitalini na kuna wale waliokimbilia maeneo salama wakiwa wametengenishwa na watoto wao ambao pia huenda wanataabika kwa ukosefu wa chakula huku wakiishi bila mama zao.

Ukosefu wa chakula ni njia ya kinyama sana ya kuaga dunia kwasababu mwili unaotaabika kwa utapiamlo unadhuru viungo vyake wenyewe ili kupata nishati ya kutosha kuendelea kuishi.

The war in Tigray broke out in November

CHANZO CHA PICHA,AFP

Wale wanafariki dunia kwanza wanakuwa ni watoto – hasa theluthi mbili ya wale wanaofarikid unia kwasababu ya baa la njaa.

Kulingana tu na takwimu zilizotolewa na Tigray, inahofiwa kwamba watoto 300,000 wamefariki dunia ikiwa ni sawa na nusu ya idadi ya watoto ambao hawajiunga na shule huko Uingereza.

Kulingana na Tigray, utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Ubelgiji cha Ghent, kati ya watu milioni 6 wa Tigray:

•Theluthi moja wanaishi maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Ethiopia

•Theluthi moja wengine wapo katika maeneo yaliyokaliwa na jeshi la Eritrea, ambalo ni washirika wa jeshi la Ethiopia, lakini halishirikiani na mashirika ya kutoa misaada

•Wengine milioni 1.5 zaidi wanaishi maeneo ya vijijini yanayodhibitiwa na waasi wa Tigray, ambapo wafanyakazi wa kutoa misaada hawawezi kufika na pia mawasiliano ya simu za mkononi yamekatizwa.

Serikali inasema kuwa inakabiliana na waasi wa Tigray na hivi karibuni itakuwa imechukuwa udhibiti kamili.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa inatabiri kuwa hali hilo itaendelea kuzorota zaidi.

The conflict in Tigray has forced hundreds of thousands of people from their homes

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kulima usiku

Katika meza ya mazungumzo, msimamizi wa USAid Samantha Power alizungumzia kile alichokiita “majaribio ya kuficha ukweli na serikali ya Ethiopia”.

Wafanyakazi wa kutoa misaada ya binadamu wana wasiwasi na mvua inayendelea kunyesha kote Tigray, ambapo wakulima walitakiwa kuendeleza shughuli zao za kilimo lakini sasa hivi imekuwa haiwezekani.

Timu ya chuo kikuu cha Ghent, hadi mwaka jana ilikuwa inafanyiakazi miradi ya kilimo katika eneo hilo na imeelezea vile maeneo makubwa ya kilimo yanavyotelekezwa mwaka huu kwasababu wakulima hawana mbegu, ngombe wa kulima waka mbolea.

Mbaya zaidi ni kwamba wanajeshi wanawatishia: “Hamutalima, hamutavuna na ikiwa mutajaribu kufanya hivyo tutawaadhibu.”

Katika maeneo ya vijijini, wakulima wanatumia ngombe wao wa wakulima kuendeleza shughuli za kilimo usiku kwenye giza kabla hakujakucha huku kukiwa na wengine wanaoangalia kwa makini kufuatilia kama wanajeshi wanavamia.

Ikiwa hakutakuwa na chakula mwaka huu, raia wa Tigray watategemea chakula cha msaada – au watafariki dunia kwa baa la njaa.

Hili ni baa la njaa lililotokana na mwanadamu.

Eneo hilo lilitambuliwa kama la mpakani “lenye chakula cha kutosha” miezi saba iliyopita, kabla ya kutokea kwa mapigano kati ya Tigray People’s Liberation Front (TPLF) – chama kilichokuwa madarakani eneo hilo – na serikali ya Ethiopia inayoongozwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Chakula kinaibwa

Vita vilivuruga utoaji wa huduma eneo hilo, benki zikafungwa na serikali ikafunga mfumo wake wa utoaji huduma za dharura.

Sehemu kubwa ya Tigray yenye mbolea ilikaliwa na wanajeshi kutoka eneo jirani la Amhara, na kuwaondoa raia wa Tigray katika mashamba yao.

Vikosi vya Eritrea ambavyo vilijiunga na mgogoro huo vimeshutumiwa kwa kuendeleza uporaji pamoja na wanajeshi wa Ethiopia, kuchoma mazao, kuharibu vituo vya afya na kuzuia wakulima kuendeleza shughuli za kilimo katika mashamba yao.

Shirika la Uhifadhi la Umoja wa Mataifa linakadiria kuwa manusura 22,000 wa ubakaji watahitaji msaada. Hofu ya unyanyasaji wa ngono kuna maanisha kuwa wanawake na wasichana wataendelea kusalia mafichoni wakiwa hawawezi kujitokeza kutafuta chakula.

Mshirika ya kibinadamu yamekuwa na mwendo wa kinyonga kujibu, kwasababu ya ukosefu wa usalama na mchakato mrefu wa urasimu umekuwa kikwazo. Kuendeleza shughuli katika eneo hili, wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wanahitaji kuwa na vifaa vya mawasiliano.

Umoja wa Mataifa unadai kwamba usambazaji wa misaada umefikia watu milioni 2.8.

Na pia kuna taarifa kwamba misaada inayotolewa kwenye malore inaibwa na wanajeshi.

Baadhi ya wanavijiji wameripoti kuwa wanajeshi wa Eritrea hujitokeza punde tu misaada inaposambazwa na kuchukua vyakula walivyopewa wakazi.

There are fears that many children will spend the rest of their lives as refugees

CHANZO CHA PICHA,AFP

Makadirio ni kwamba asilimia 13 ya watu milioni 5.2 wanahitaji msaada.

Wafanyakazi wa kutoa misaada wameuawa – wa hivi karibuni ikiwa ni Mei 28. Jeshi la Ethiopia kawaida huwa linazuia wafanyakazi wa kutoa misaada kufika maeneo ya vijijini na kuwashutumu kwa kusaidia waasi.

Maafisa wa eneo wanadai kwamba pande zote katika mapigano hayo zimejihusisha na uporaji. Hata hivyo ripoti ya Umoja wa Mataifa imeripoti matukio 129 ya ukiukaji wa haki za binadamu yaliyotekelezwa na Wanajeshi wa Ethiopia na wa Eritrea.

Ombi la kusitisha mapigano

tigray

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Pia kuna makubaliano ya kile kinachohitajika kufanywa kukabiliana na hali hiyo – lakini kwa sasa hivi, muda umepita kusitisha mapigano hayo.

Makubaliano hayo yanajumuisha kusitishwa kwa uchokozi kati ya pande mbili, kulinda raia walio katika hatari ya kuathirika na ghasia hizo ikiwemo ubakaji na kuzuia kufikiwa kwa misaada.

Hakuna kilicho wazi. Wiki jana, msemaji wa serikali ya Ethiopia alisisitiza kuwa operesheni za kijeshi zitafikia ushindi mkubwa na kuondoa suala la makubaliano ya kusitisha vita.

‘Musisubiri kuhesabu makaburi’

Mashirika ya kutoa misaada yamevumbua njia za kuendeleza shughuli zao katika maeneo ya vita – lakini yanahitaji ushirikiano kutoka pande zote.

Many people have struggled to get medical treatment in Tigray

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hakuna ishara ya kufikiwa kwa hilo, huku serikali ya Ethiopia ikisisiiza kwamba waasi ni “magaidi” na hakuhitajiki kuwa na ushirikiano au makubaliano yoyote nao, hata katika masuala ya kunusuru maisha ya watu.

Mashirika ya kutoa misaada huko Tigray yanaendelea kuongezeka lakini mabadiliko yanafanyika kwa mwenzo wa kinyonga kufikia yanayohitajika.