Thursday, January 9

MAKALA VIDEO: SAUTI YAO, jee! unataka kujua leo itasikika sauti ya nani katika makala haya?

 

NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.

Kukomesha umaskini wa mtoto ni muhimu sana kwa ajili ya kutoa haki kwa kila mtoto na kwa ajili ya mustakabali wa jamii na Taifa kwa ujumla.

Ikiwa hautashughulikiwa kwa ukamilifu, umaskini utawazuia watoto kufikia ukuaji wao kamili na kudumaza ustawi wa taifa, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya ‘Dira ya Tanzania ya mwaka 2025′.

Ili kupima umaskini wa mtoto kwa ufanisi, mahitaji mengine muhimu kwa ajili ya ustawi wa mtoto, mbali na kipato cha kaya, yanatakiwa kujumuishwa.

Hivyo,Tanzania imeandaa njia ya kupima umaskini wa mtoto kwa ukamilifu ambayo ni mahsusi kwa nchi.

Kipimo hicho kinazingatia uwezekano wa mtoto kupatalishe, huduma za afya, ulinzi na usalama, elimu, habari, usafi wa mazingira, maji na makaazi.

Upimaji sahihi wa umaskini wa mtoto ni muhimu sana nchini Tanzania kwa kawaida dira ya watoto inatarajiwa kuongezeka kwa kasi hadi kufikia mwaka 2030.

Pamoja na upimaji huo bado katika Visiwa vyetu vya Unguja na Pemba kuna baadhi ya kaya ambazo zinakabiliwa na umasikini uliokithiri ambao kwa kiasi Fulani unahitaji kusaidiwa.

Kwani Watoto wa familia hii ambayo tunaizungumzia wako hatarini kukosa elimu, lishe bora na hata maakazi kutokana na mazingira yao ya maisha yalivyo.

Iwapo  hali hii haikuzingatiwa kwa kuwapa msaada ipasavyo itasababisha kurudisha nyuma malengo hayo.

Ilikujua hali halisi ya mazingira duni kwa watoto katika  kaya hii ungana nami katika kuingalia  makala hii.

 

KUANGALIA MAKALA HII BOFYA VIDEO HAPO CHINI