NA KHADIJA KOMBO -PEMBA.
Huruma inatokana na Imani na Imani ndio msingi Mkuu wa Dini ya Kiislam hivyo katika dini tumehimizwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwahurumia na, kusaidiana kwahali na mali kwani muislam ndugu yake ni muislamu mwenziwe.
Hivyo katika mzunguko wetu wa Maisha umekuwa ukikumbana na mambo mengi , katika mazingira yetu tunayoishi wengine ni masikini wengine ni wagonjwa wengine ni yatima na wengine ni wazee wasiojiweza hivyo kutokana na msingi wa dini yetu tunapaswa kuwaonea huruma watu hao na kuwa nao bega kwa bega.
Na leo basi katika Makala hii fupi tuna waangalia watoto yatima ambapo yatima ni yule mtoto alie ondokewa na wazee wake wawili au mmoja wao, huyu ana haja kubwa ya kuonewa huruma, kusaidiwa na kuongozwa tangu udogo nakufunzwa adabu na tabia njema.
Na ikiwa atakosa haya, bila ya shaka atainukia katika tabia mbaya na atakuwa na mtazamo wa chuki kwa jamii yake kwa sababu ya kumtupa na kumdharau.
Ili kulinusuru hilo Ustadh Khamis Mbwana kutoka Micheweni yeye kwa upande wake ameamua kuwaweka pamoja baadhi ya yatima kwa kufungua kituo maalum cha watoto yatima na kuwahudumia kwa hali na mali huku akichukua juhudi ya kuwafunza dini yetu ya kiislam kwa kuwasomesha Quran pamoja na mambo mengine ya dini kupitia hapo hapo madrasa.
Katika kumuunga mkono Ustadh Khamis Mbwana , Wadau mbali mbali wamekuwa wakijitokeza katika kuwasaidia na kuwafariji watoto hao. Jee ninani ambao wameweza kuitikiya wito huo wakusaidia yatima hao ungana nasi katika Makala hii.
KUANGALIA MAKALA HII BOFYA VIDEO HAPO CHINI.