Thursday, January 9

MASHINDANO ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete

WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Piki wakiimba wimbo katika mashindano ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete huko katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Mchangamdogo Pemba.(PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)

NA SAID ABDULRAHMAN.

 

MASHINDANO ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete, yaliendelea tena mwishoni wiki lililopita kwa upande wa michezo ya sanaa na maigizo.

 

Mashindano hayo ambayo yalifanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Mchangamdogo, yaliweza kuzikutanisha Skuli zote msingi na Sekondari zilizomo katika Wilaya hiyo.

 

Katika ngarambe hizo Skuli ambazo zimeshinda nafasi ya kwanza na ya pili, zitaweza kuiwakilisha Wilaya ya Wete kwa ngazi ya Mkoa ambapo wataweza kushindana na mabingwa wenzao wa Wilaya ya Micheweni.

 

Michezo iliweza kushindaniwa ni pamoja na Ushairi, Utenzi, Wimbo, Tamthilia na mdahalo.

 

Kwa upande wa Ushairi, washindi ni Skuli ya msingi Kisiwani walipata alama 275 sawa na asilimia 91.66%, mshindi wa pili skuli ya Kizimbani iliyopata alama 244 sawa na asilimia 81.33%.

 

Kwa upande wa Sekondari, Wete Sekondari iliweza kupata nafasi ya kwanza baada ya kupata alama 254 sawa na asilimia 84.66% huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Idrisa Abdulwakil kwa kupata alama 244 sawa na asilimia 81.35%.

 

Kwenye Utenzi, Minungwini msingi iliweza kushika nafasi ya kwanza baada ya kupata alama 256 sawa na asilimia 85.33%, huku Bwagamoyo ikapata nafasi ya pili baada ya kupata alama 254 sawa na asilimia 84.40%.

 

Sekondari Utenzi, washindi ni Kijumbani ambapo ilijipatia alama 281 sawa na asilimia 94.22%, Mchangamdogo wakipata nafasi ya pili baada ya kupata alama 250 sawa na asilimia 83.33%.

 

Ama kwa upande wa wimbo, msingi washindi ni Skuli ya Piki ambayo ilipata alama 269 sawa na asilimia 89.66% huku Kangagani ikipata nafasi ya pili baada ya kupata alama 257 sawa na asilimia 85.66%.

 

Kwa upande wa Sekondari, washindi ni Kangagani ikipata nafasi ya kwanza baada ya kupata alama 273 sawa na asilimia 91.00% huku Gando ikishikilia nafasi ya pili baada ya kupata alama 255 sawa na asilimia 86.00%.

 

Ngonjera Skuli msingi ni Jadida, ilishika nafasi ya kwanza baada ya kupata alama 239 sawa na asilimia 79.88%, Mgogoni msingi ikipata nafasi ya pili baada ya kupata alama 179 sawa na asilimia 59.00%.

 

Kwa upande wa Sekondari, Chasssa Sekondari iliweza kupata alama 251 sawa na asilimia 81.66% na kushikilia nafasi ya kwanza huku Mchangamdogo ikipata alama 229 sawa na asilimia 76.00% na kuwa mshindi wa pili.

 

Ama kwa upande wa Tamthilia msingi, washindi ni Skuli ya msingi Bopwe ambayo ilipata alama 199 sawa na asilimia 66.18% na kushika nafasi ya kwanza huku Mchangamdogo ikipata nafasi ya pili kwa kupata alama 55.74%.

 

Kwa upande wa Sekondari, Idrisa Abdulwakil ilishikilia nafasi ya kwanza baada ya kupata alama 235 sawa na asilimia 78.33% huku Mchangamdogo ikiwa nafasi ya pili baada ya kupata alama 221 sawa na asilimia 73.61%.

 

Kwa upande mdahalo, Wete Sekondari ilishika nafasi ya kwanza baada ya kupata alama 158 sawa na asilimia 78.00% huku Uondwe ilishika nafasi ya pili kwa kupata alama 158 sawa na asilimia 75%.

 

Mapema akifungua mashindano hayo afisa elimu Sekondari Wilaya ya Wete Riziki Makame Faki, aliwataka wanafunzi hao kushiriki katika michezo mbali mbali ili Kujenga afya zao, wanafunzi kuweka nidhamu wakati wote wa Mashindano wakati yakiendelea.