Monday, November 25

VIDEO: Serikali kuandaa mikakati maalumu kwa mwanamme atakaetelekeza familia yake.

NA SHEKHA SEIF –PEMBA.

Kamati za kupinga udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kisiwani Pemba wameiyomba Serikali kuandaa mikakati maalum itakayomkabili mwanamme atakaetelekeza familia yake ili waweze  kupeleka huduma zinazo stahiki kwa familia hiyo.

Hayo wameyasema huko katika ofisi ya Tamwa Mkanjuni Chake Chake Pemba wakati walipokuwa katika  mkutano wa kujadili changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao.

Wamesema endapo Serikali itaandaa mikakati hiyo na kuisimamia ipasavyo itapunguza kesi hizo na kuondokana na utelekezaji wa wanawake na watoto jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya taifa .

Aidha wanakamati hao wameitaka jamii kuiunga mkono katika kuibua kesi za utelekezwaji wa wanawake na watoto kwa lengo la kuzisaidia familia zilokumbwa na nakadhia hiyo.

Mapema akifungua mkutano huo Mratibu wa Tamwa Pemba Fat-hiya Mussa Said amewashukuru na kuipongeza kamati hiyo kuwa na msimamo wa pamoja katika kusimamia kesi hizo .

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI