Friday, January 10

HABARI PICHA: MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.

WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Kizimbani wakiimba wimbo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,

WANAFUNZI wa Skuli pamoja na wadau mbali mbali wakiwa katika matembezi katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib akipokea maandamano ya wananchi katika kilele Cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, (Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni Yahya Khatib akiongoza maandamano hayo)

 

 

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete

 

MKUU wa Wilaya ya Wete Mgeni Yahya Khatib akiwahubia wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,

WANANCHI Kisiwani Pemba wakiwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
AFISA Mdhamini Wizara ya afya Pemba Yakoub Shoka akitoa maelezo mafupi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
AFISA kutoka Idara ya Ustawi wa jamii Pemba Bizume Haji akitoa maelezo katika kilele Cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,
WASANII wakionesha onesho lao katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,

(PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)