Tuesday, November 26

Leo, Juni 16 Tanzania Inaungana na Mataifa Mengine Kimataifa Kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani.

Siku hii ambayo chimbuko lake ni kumbukumbu ya watoto zaidi 2000 waliuawa wakati wakiandamana kupinga ubaguzi wa rangi katika mfumo wa elimu nchini Afrika Kusini mnamo mwaka 1976.

Maadhimisho hayo kwa hapa nchini Tanzania yanafanyika katika ngazi ya Halmashauri ili kuwawezesha wananchi kwa wingi wao kushiriki maadhimisho hayo.
*Mkoani Dodoma, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inaungana na Mkoa huo kuadhimisha Siku hiyo ambapo pamoja na mambo mengine, Makamu wa Rais, Dkt. Philip  Mpango atazindua Makao ya Taifa  ya Watoto- Kikombo yanayolenga kuwahudumia watoto walio katika mazingira magumu.
Makao hayo yenye uwezo wa kuhudumia watoto 250 kwa wakati mmoja yamejengwa kwa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Abbott.
Mwaka huu kaulimbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika inasema, “Tutekeleze ajenda 2040: kwa Afrika inayolinda haki za mtoto”