Friday, January 10

VIDEO: Wasimamizi wa uchaguzi katika uchaguzi mdogo Jimbo la Konde watakiwa kufanya kazi kwa kufuata sheria ya Tume.

NA KHADIJA KOMBO -PEMBA                             

Makamo Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Taifa  (NEC)  Bwana Mbarouk Salim Mbarouk amewataka wasimamizi wa uchaguzi katika uchaguzi mdogo Jimbo  la Konde kufanya kazi kwa kujiamini na uweledi huku wakifuata sheria na maelekezo kutoka TumeyaUchaguzi Taifa.

Makamo Mwenyekiti huyo ametoa wito huo huko katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watendaji hao juu ya namna ya kutekeleza kazi hiyo kwa ufanisi.

Amesema kuvifahamu vituo mapema , kushirikiana na vyama vya siasa pamoja na wadau wengine ni miongoni mwa  mambo muhimu ambayo yatasaidia kufanikisha kazi hio.

Mapema watendaji hao walikula kiapo juu ya uaminifu wa kutekeleza majukumu hayo.

Uchaguzi mdogo Jimbo la Konde unatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 18/7/2021

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI.