Monday, November 25

Jamii imetakiwa kuacha kuwaficha wahalifu wanaowafanya matukio ya udhalilishaji wa kijinsia na kuzifanyia suluhu majumbani kesi hizo.

 

NA FATMA HAMAD -PEMBA .

Jamii imeonywa kuacha tabia yakuwaficha wahalifu wanaowafanya matukio ya udhalilishaji wa kijinsia na kuzifanyia suluhu kesi za hizo majumbani jambo ambolo linapelekea kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji.

Akizungumza na Wazazi na Walezi katika mkutano wa kuielimisha jamii juu ya athari za udhalilishaji katibu wa kamati ya madili Zanzibar Abdala Mnubi Abass huko Tumbe wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema vitendo vya udhalilishaji vinajitokeza siku hadi siku, lakini bado jamii inaonekana ikizifumbia macho na  kuzifanyia suluhu kesi hizo wenyewe kwa wenyewe.

‘’ wakishafanya makosa ya udhalilishaji mna watorosha watoto wenu, wazazi wacheni hii tabia, Alisema Abdala Mnubi’’.

Amesema wengi wafanyaji wa matukio hayo ni watu wa karibu katika familia, hivyo wazazi wanapodhalilishiwa watoto wao wasiwaonee haya wala wasiogope maneno ya mitaani bali wasimame kidete  na kuwaripoti katika vyombo vya sheria ili kuchukuliwa hatua kali dhidi yao.

Hata hivyo Mnubi amewaasa watoto wasikubali kupokea zawadi au kitu chochote watakachopewa na watu njiani jambo ambalo litawaepusha na udhalilishaji.

Baadhi ya wazazi walioshiriki mkutano huo wamesema nivyema Jamii kushirikiana katika malezi ya pamoja kama ilivyokua zamani ili kupata kizazi chenye madili bora.