(PICHA NA ABDI SULEIMAN.PEMBA)
NA ABDI SULEIMAN.
WIZARA ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, imetoa wiki mbili kwa uongozi wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) kuhakikisha wanaikamilisha na kukabidhi miradi yote ya ajira kwa vijana ya Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa katika ubora wake.
Miradi hiyo ni visima vya maji kuongezwa urefu na kufungia vifaa vyake ikiwemo upelekaji wa umeme na baadhi ya Green House kutokuwa na viwango huku nyengine zikiwa mbovu.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Zanzibar, Fatma Hamad Rajab mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kukagua visima na Green House hizo Mkoani Kusini Pemba, akifuatana na watendaji wa wizara hiyo Unguja na Pemba, watendaji kutoka JKU Zanzibar ndio waliopewa tenda ya ujenzi wa visima na Green House, Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema lengo la ziara ni kukagua miradi hiyo na kukabidhiwa Serikali, lakini kutokana na kutokufikia viwango na malengo ya mikataba, Wizara haiko tayari kuipokea mpaka pale itakapokamilika, kwani imegharimu fedha nyingi za serikali katika utekelezaji wake.
Alifahamisha kuwa lengo la serikali ni kuwapelekea vijana miradi hiyo, nikuona jinsi gani itaweza kuwakomboa kiuchumi na kuwainua kimaendeleo, lakini kutokana na changamoto hizo itakuwa ni mzigo kwa vijana kuwapatia ikiwa haijakamilika kiwango.
“Miradi hii ni utekelezaji wa ajira kwa vijana ile ya Bilioni 3 za Serikali ya awamu ya saba ya Dkt.Shein, ilioanza 2018 na ilitakiwa tuikabidhiwe muda huu, lakini sisi hatuipokei mpaka pale malengo yake yatakapofikiwa ikiwemo kufikia viwango”alisema.
Aidhja Katibu Mkuu huyo alisema, Wizara haiko tayari kuona fedha za serikali ambazo zimetolewa kwa lengo la kuwasaidia vijana, vinapotea na kuwanufaisha watu wachache kwa maslahi yao watahakikisha fedha hizo zinarudishwa au miradi inakamilikwa kwa viwango vilivyokusudiwa.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa JKU kuhakikisha wanashirikiana na ZAWA katika suala la visima vya maji kwani ndio watalaamu wa maji Zanzibar, ili kuona maji yanapatikana kwa umakini.
Naye katibu tawala wilaya ya chake chake chake Omar Juma Ali, alisema kwa upande wa Wilaya hawatakua tayari kukabidhiwa miradi ambayo haina ubora wala viwango, kwa ajili ya vijana mapaka pale wizara husika itakapojiridhisha katika miradi hiyo.
Alisema serika ilikuwa na nia safi ya kuwaendeleza vijana nchini, lakini juhudi zao zake zimeanza kupotea kidogo kidogo, huku vijana wakianza kukata tama ya kunufaika na miradi hiyo.
“Baada ya Wizara kuipokea kutoka JKU, Wizara itatukabidhi sisi na sisi tunataka kuona miradi hiyo iko katika viwango vya juu, hii inakuwaje Taasisi inashindwa kupika wilaya kuonyesha mpango kazi wake na inafika vijijini”aliseka.
Kwa upande weake Mkuu wa Mkuu wa Kilimo kutoka JKU Zanzibar Ramadhan Ali Hassan, alisema kutokuwepo kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya miradi, kumesababisha kushindwa kuvijaribu visima hivyo, ili kuhakikisha vinamaji ya kutosha kukidhi mahitaji ya kilimo.
Aidha alikiri kuwepo kwa changamoto katika baadhi ya miradi iliyotekelezwa na kutokufikia viwango, huku akiahidi kuhakikisha miradi hiyo wataifanyia matengenezo na kuona inakabidhiwa kwenye wizara husika.
Mapema upande wao baadhi ya vijana ambao wamejengewa visima na green house, wameitaka wizara kuhakikisha wanakutana na uongozi wa JKU, ili kuona miradi inakamilika na vijana wanakabidhiwa kwa lengo la kujikomboa na umasikini.
Mapema Viongizo hao walifika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba kwa lengo la Kujitambulisha, huku akiwataka viongozi hao kuwa serikali ya Mkoa huo hautakua tayari kupokea miradi ambayo haijakamilika katika lengo lililokusudiwa.
Alisema serikali imeahidi kwa vijana kuwapatia ajira, leo miradi hiyo imeshindwa kukamilika hiyo kitendo hicho hatokifumbia macho ikizingatiwa miradi hiyo imegharimu fedha nyingi za serikali.