NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Wahenga wanasema Chanda chema huvikwa pete ikiwa na maana ya kwamba unapofanya jambo jema basi daima na wewe utalipwa mema na wengine wakadiriki kusema kwamba mcheza kwao hutunzwa yote hayo ni katika kusisitiza kufanya kila lililo jema ili hatimae na wewe uweze kupata wema.
Na katika kudumisha huo wema wengine wakasema deni la ikhsani hulipwa kwa ikhsani ikiwa na maana ya kwamba kamwe usikubali kwa mtu anaye kufanyia ikhsani ukamlipa nuksani (maovu).
Yote haya tumeyapigia mfano kwa kumlinganisha Dr. Mohammed Haji Shaali ambaye ni Mfanyakazi ya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani tokea miaka ya 1990 ni takriban miaka 31 sasa. Na miaka yote hio alikuw aakitoa huduma kama mtaalamu wa mionzi katika hospitali hio. Mtu ambae ni Muhimu si kwa Hospitali ya Abdalla Mzee tu lakini ni muhimu kwa jamii yote..
Kutokana na umuhimu wake, Uongozi wa Hospitali ya Abdalla Mzee ulitamani sana kuwa pamoja na Dk huyu siku zote ili aendelee kuitumikia jamii. Lakini AH; ukipanga vyako na Mungu naye hupanga vyake na kwako ikawa ni kupokea tuu na kushkuru Alla kullihali. Dr Mohammed kwa sasa amepata mtihani wa maradhi tokea mwezi disemba 2018, lakini hii ni kazi yake Allah tunajuwa wazi kwamba haina makosa kwetu ni kushkuru kwani mitihani ametuumbia sisi binaadam hivyo hatuna budi kusema Alhamdulillah.
Pamoja na kumshukuru Mungu hatukupaswa kuishia hapo , juhudi zetu zilitakiwa kuonekana katika kumsaidia mwenzetu huyu pamoja na kumuombea kwa Allah ili arudi katika uzima wake .
Katika kipindi cha awali sihaba Abdalla Mzee ilimsaidia kwa hali na mali katika kipindi chote cha miezi sita alicholazwa hapo Pamoja na juhudi hizo bado Dr. Mohammed anahitaji matibabu zaidi ili hali yake iweze kutengemaa na kurudi tena katika ulingo wa kuwasaidia wananchi , ndipo alipo amua kufanya mazungumzo na Daktari bingwa wa kichina waliopo Hospitalini hapo ili waweze kuleta maarifa zaidi na hapa anajaribu kutufafanulia mazungumzo hayo.
ILI KUJUA NI SAUTI YA NANI LEO IPO HEWANI BOFYA VIDEO HII HAPO CHINI.