(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NA ABDI SULEIMAN.
MRAJISi wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla, amesema kuanzishwa kwa mradi wa Uhamasishaji wa upatikanaji wa haki za umiliki wa ardhi kwa wanawake, utasaidia sana serikali katika kupunguza tatizo la migogo ya ardhi.
Aliyaeleza hayo wakati wa alipokua akifungua kongamano la kujadili kuanzishwa sera ya kuharakisha mirathi, katika jamii ambayo ndio chanzo kikuu cha wanawake haki za kumiliki ardhi na mali nyengine, chini ya mradi unaoendeshwa Jumuiya ya kuwawezesha Jamii Pemba (PECEO), kwa Ufadhili wa The Foundation for civil society na kufanyika mjini Chake Chake.
Alisema migogoro ya ardhi mara nyingi husababishwa na wananchi, wakiwemo wakubwa wenye fedha zao hivyo makongamano kama hayo yanasaidia sana kuelimisha jamii.
“Wanawake wanaingia katika ndoa na panapotokea migogoro, inapelekea kukosa haki zao au familia zao kuanza kuwabana na kuwapa visingizio kadhaa”alisema.
Aliwataka wanawake kuhakikisha wanafahamu haki zao, pamoja na kuhakikisha PECEO elimu hiyo inafika kwa jamii yote ikiwemo wanawake walioko vijijini.
Mrasiji wa NGOs Zanzibar alisema serikali inajitahidi katika kusaidia NGOs kwa kuziweka mazingira bora na rafiki, ili kuhakikisha NGOs zinafikia malengo yake.
Akiwasilisha mada ya Mirathi katika Uislamu Shekha Said Ahmad kutoka Ofisi ya Mufti Pemba, aliwataka wananchi wasikimbilie kurithi mpaka watakaposhuhulikia madeni ya marehemu.
Alisema uislamu umesimamia suala la mirathi inafanyika, kwa lengo la kuondosha migogoro pale mmoja ya wanafamilia anapofariki, lakini jambo la kusikitisha suala hilo linacheleweshwa na kupelekea tatizo na kuongezeka kwa migogoro katika jamii.
“Tunapaswa kujifunza kutokana na makosa yanayotokea, pale mwenzetu anapofarikia kinachofuata ni suala la mirathi na sio vyenginevyo, ila suala la migogoro ya ardhi imekua ni mengi sana”alisema.
Aidha aliipongeza Jumuiya ya PECEO kwa kuandaa kongamano la kujadili kuanzishwa sera ya kuharakisha mirathi, kwani kupatikana kwa sera hiyo suala la mirathi itakuwa sio hiyana badala yake ni jambo la kisheria na kisera na kupelekea wanawake kupata haki zao.
Katibu wa Mradi wa Uhamasishaji wa upatikanaji wa haki za umiliki wa ardhi kwa wanawake, kutoka PECEP Juma Said alisema inafika miaka 10 hadi 15 baada ya mmoja ya wanafamilia kufariki bado mali zinaendelea kutumiwa kifamilia baada ya kurisishana.
Wakichangia katika kongamano hilo, baada ya wadau waliishauri PECEO kuandaa vipeperushi mbali mbali kwa ajili ya kuwapatia wananchi hususana walioko vijijini.
Time Mohamed Shaame aliitaka PECEO kuzungumza na watendaji wa kamisheni ya ardhi, kwani suala la usajili wa ardhi limekua ni gharama kubwa.
Asia Amor alisema wananchi wanahitaji sera ya mirathi ili wanawake waweze kupata haki zao, sambamba na kuendelea kuelimisha wananchi wengine.