Monday, November 25

VIDEO: CRDB yazindua Jumuiya ya waendesha boda boda mkoa wa kusini Pemba (Pesboa).

KHADIJA KOMBO – PEMBA.                 

Waendesha boda boda katika Mkoa wa kusini Pemba wametakiwa kuafuata sheria za bara barani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Akizungumza na waendesha boda boda hao huko katika Viwanja vya Polisi Madungu Chake Chake katika uzinduzi wa Jumuiya ya waendesha boda boda mkoa wa kusini Pemba (Pesboa) ikiwa chini ya Benk ya CRDB , Mkuu wa Mkoa huo Mh. Mattar Zahor Massoud amesema hivi sasa kumekuwa na ajali nyingi za bara barani na wakati mwengine hupoteza maisha ya watu na ukiangalia chanzo chake ni usafiri wa boda boda.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba ACP Richard Tadei Mchovu amewataka wana jumuiya hao kuepuka kutumiwa na watu waovu katika kuwasaidia kufanya uhalifu.

Akizungumzia kuhusu usalama barabarani  RTO Shawal Abdalla Ali amesema maafa yanayotokea barabarani mara nyingi hutokea kutokana na madereva hao kutokutii sheria za barabarani hivyo amewataka kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa na lazima.

Naye Meneja Tawi la Benk ya CRDB Pemba Mustafa Kambi amesema Benk yake imeamua kushajihisha kuanzisha jumuiya hio kwa lengo la kusaidia kuinua hali zao kiuchumi lakini  pia kudhibiti maafa yanayotokea kutokana na usafiri huo.

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI