Mnamo tarehe 23 Juni 1993 mke mchanga alikata uume wa mumewe katika shambulio lililowashangaza wnegu . Mke huyo alikuwa Lorena Bobbitt – na mume wake alikuwa John Wayne Bobbitt – na kisa hicho kilizungumzia kote duniani .
Kwa wale wanaokumbuka, kisa hicho ,kumbukumbu hizo bado zipo na siku kama hii ya leo ambapo ulimwengu unaadhimisha siku kupambana na dhulma za kijinsia. Kisa cha Lorena Bobbit na mume wake John kinaleta vyema taswira ya jinsi dhulma katika ndoa au uhusiano zinavyoweza kugeuka na kuwa kitu kibaya zaidi au hata maafa .
Miaka ishirini na nane iliyopita, huko Manassas, Va., Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 alikata uume wa mumewe na kisu cha jikoni.
Jina lake lilikuwa Lorena Bobbitt. Kilichofuta na habari za tkio hilo kugonga vichwa vya habari nchini Marekani na kote duniani na kulifanya jina Bobbit kupata umaarufu usiotarajiwa .
Ilikuwa ni juni mwaka wa 1993 wakatia Lorrena aliojpata ameuteka ulimwengu kwa habari za kitendo chake cha kumkata uume mume wake.Mwanadada huyo mhamiaji kutoka Ecuador ambaye alikulia Venezuela alidai kwamba mume wake John Wayne ambaye alikuwa mwanajeshi hapo awali alikuwa akimbaka .akini ilichukua muda mrefu mrefu kwa ulimwengu kuwa tayari kusikiliza upande wake wa masimulizi .
Nini kilichofanyika?
Lorena Bobbitt alisema kortini kwamba, baada ya kurudi nyumbani jioni hiyo, mumewe alimbaka. Baada ya yeye kulala, aliinuka kitandani na kwenda jikoni kunywa maji. Kisha akachukua kisu cha inchi 8 kwenye kaunta ya jikoni, akarudi chumbani kwao, akavuta shuka na akakata uume wake.
Baada ya hayo, Lorena aliondoka katika nyumba hiyo na uume aliokata na kusafiri kwa gari lake. Baada ya kuendesha gari kwa muda na kujitahidi kuliekeleza kwa mkono mmoja, aliitupa nje ya dirisha kwenye uwanja kando ya barabara. Mwishowe alisimama na kupiga simu ya 9-1-1, akiwaambia kile kilichotokea na mahali ambapo uume ungeweza kupatikana. Uume wa John Bobbitt ulipatikana baada ya kusakwa kwa muda mrefu . Baadaye alioshwa na dawa ya kuzuia vimelea na kuingizwa kwenye barafu ya chumvi, kisha sehemu yake hiyo ikarejeshw akatika mwili wake kwenye oparesheni iliyodumu maasa tisa na nusu .
John alipona na hata baadaye kuigiza katika filamu mbili za ponografia miaka ya 1990, na akasema mnamo 2018 kwamba uume wake “umerudi katika hali ya kawaida”.
Kesi iliyofuata
Lorena Bobbitt alipokamatwa usiku wa Juni 23, aliwaambia polisi, “Yeye huwa na hamu ya ngono kila wakati, na hanisubiri nipate mshindo. Yeye ni mbinafsi.” Mazungumzo haya na Mpelelezi Peter Wentz yalirekodiwa kwa kanda, na nakala hiyo ilisomwa baadaye katika kesi hiyo na Mary Grace O’Brien, Wakili aliyesimamia kesi ya kumshtaki Lorena.
Wakati wa kesi, wawili hao alifichua maelezo ya uhusiano wao tete na matukio ambayo yalisababisha shambulio hilo. Lorena alisema kuwa John alimnyanyasa kingono, kimwili, na kifikra wakati wa ndoa yao.
Mawakili wake wa utetezi, ambao walikuwa pamoja na wakili wa utetezi Blair D. Howard, walisisitiza kwamba unyanyasaji wake wa kila mara mwishowe ulimfanya “aichukue hatua kali” kwa sababu alikuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo .
John alikanusha madai ya unyanyasaji; walakini, alipoulizwa maswali na Howard, taarifa zake mara nyingi zilikinzana na ukweli unaojulikana, na kudhoofisha sana kesi ya upande wa mashtaka.
John Bobbitt baadaye aliachiliwa huru wamauzi waliojuisha wanawake tisa na wanaume watatu kwa madai ya ubakaji . Alikuwa na masimulizi tofauti kuhusu kile kilichotokea jioni hiyo inayozungumziwa, akielezea kwa nyakati tofauti kwa polisi na kortini kwamba “hawakushiriki ngono; kwamba Lorena alijaribu kuanzisha ngono, lakini alikuwa amechoka sana; kwamba walikuwa wakishiriki ngono, lakini alikuwa amelala.
Baada ya masaa saba ya kujadili, majaji walipata Lorena hana hatia kwa sababu ya uwendawazimu wa muda na kusababisha msukumo usioweza kushikiliwa wa kumjeruhi John kingono. Kama matokeo, hakuweza kuwajibika kwa matendo yake. Chini ya sheria ya serikali, jaji alimwamuru apitie siku 45 za matibabu na uangalizi katika Hospitali Kuu ya Jimbo, Petersburg, Virginia, na baada ya hapo aliachiliwa huru . Mnamo 1995, baada ya miaka sita ya ndoa, John na Lorena walitalakiana
Maisha ya baadaye
Baada ya tukio hilo, John alijaribu kujipatia pesa kutoka kwa umaarufu wake kwa kuunda bendi, The Severed Parts, kulipa ada yake ya matibabu na ya kisheria, ingawa bendi haikufanikiwa na ilishindwa kupata pesa za kutosha. Mnamo Septemba 1994, alionekana kwenye filamu ya watu wazima John Wayne Bobbitt: Uncut, katika jaribio lingine la kupata pesa. Mnamo 1996, alionekana katika filamu nyingine ya watu wazima, Frankenpenis (pia inajulikana kama Frankenpenis ya John Wayne Bobbitt).
Mnamo 1994, alishtakiwa kwa kumpiga Kristina Elliott, mchezaji wa zamani wa densi mwenye umri wa miaka 21 aliyekutana naye huko Las Vegas kwenye ziara
Baada ya kesi hiyo, Lorena alijaribu kuishi maisha ya siri na akarejelea matumizi ya jina lake la kuzaliwa, Gallo. Mnamo Oktoba 1996, alitembelea nchi yake ya asili Ecuador, ambapo alikutana na rais wa wakati huo Abdalá Bucaram kwa dhifa ya chakula cha jioni.
Bucaram alikosolewa kwa kumwalika Lorena kwenye dhifa hiyo ya chakula cha jioni
Mnamo Desemba 1997, aligonga vichwa vya habari wakati aliposhtakiwa kwa shambulio baada ya kumpiga mama yake, Elvia Gallo, walipokuwa wakitazama runinga. Mwishowe aliachiliwa huru kwa shambulio hilo na kuendelea kuishi na mama yake. Mnamo 2007, alikuwa akifanya kazi katika saluni huko Washington, D.C. na katika mwaka huo huo ilianzisha shirika la Red Wagon la Lorena, ambalo husaidia kuzuia unyanyasaji wa nyumbani kupitia shughuli zinazohusu familia.