Monday, September 16

Oparesheni Barbarossa: Maswali 10 ya kuelewa ‘kosa baya zaidi’ la Hitler katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia

Maelezo ya picha,Propaganda ilikuwa kiungo muhimu katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Wasovieti kama inavyoonekana katika picha hii , walijaribu kuweka ari juu katika kupinga uvamizi wa Nazi

Mnamo Juni 22, 1941, Wanazi wa Ujerumani walizindua oparesheni Barbarossa, dhidi ya Muungano wa Soviet ambayo wakati huo ilikuwa ikiongozwa na José Stalin.

Ulikuwa uvamizi mkubwa wa kijeshi katika historia, na dau hatari ambalo Adolf Hitler alitumia kubadili hatma ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kwa maslahi yake.

Lakini mambo hayakuenda kama alivyopanga, na wanahistoria wanachukulia kufeli kwa oparesheni hiyo kuwa mwanzao wa na mwisho wa nguvu ya Ujerumani.

Operasheni Barbarossa ilikuwa mwanzo wa miezi sita ya vita vikali kati ya madola mawili ya kiimla, ambayo ingeishia kuamua matokeo ya vita.

Oparesheni hiyo ilibatizwa jina Barbarossa kwa heshima ya Frederick Barbarossa, Mfalme Mtakatifu wa Roma wa karne ya 12. Uvamizi wa Wajerumani dhidi ya Umoja wa Nchi za Usovieti wa Urusi (USSR) ambayo ni Urusi ya sasa ulivunja mkataba wa amani baina ya nchi hizo uliosainiwamnamo 1939.

Vikosi vya vilijumuisha wanaume milioni tatu waliogawanywa katika makundi matatu yaliyolenga miji ya Leningrad, Kiev na Moscow mtawalia.

Vikosi vya Usovieti vilishambuliwa ghafla na vilijeruhiwa vibaya katika mapambano ya kwanza. Mamilioni ya wanaume wanakadiriwa kufariki na miji kama Kiev, Smolensk, na Viazma kutekwa na Wanazi.

Ingawa hatua hii ilisaidia Sovieti kuimarisha ulizi wake, makali msimu wa baridi wa Urusi, pia ilifanya vikosi vya Ujerumani kupunguza kasi ya mashambulio, kufikia Disemba vikosi vya ardhini vilikuwa tayari vimeingia Moscow.

Huku hayo yakijiri, Hitler alikuwa amefanya uamuzi wa kushambulia mji wa Leingrad, na kuuzingira kwamuda mrefu.

Ijapokuwa wanajeshi wa Sovieti iliponea shambulio la kwanza, vikosi vya Ujeremani vilianzisha mashambulio mapya mwaka 1942 kuvamia maeneo zaidi ya USSR.

Ni vita vya Stalingrad, kati ya mwaka 1942 na 1943 ambavyo vilibadilisha mkondo wa mapigano na kuishia kuwarudisha nyuma Wajerumani.

Uvamizi huo uliandamana na unyanyasaji mkubwa dhidi ya raia wa Sovieti. Miongoni mwa waliathirika zaidi ni Wayahudi.

Zaidi ya Wayahudi milioni moja walifariki na suluhisho la mwisho, mpango wa Hitler ulikuwa kuwaangamizi wote.

Miaka 80 tangu uvamizi huo mwanahistoria wa Uingereza Anthony Beevor, mtaalamu wa historia ya kijeshi na Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, amejibu maswali 14 ya BBC kujaribu kuelewa makosa makubwa yaliyofanywa na Hitler.

1. Je Hitler alikuwa na mpango wa muda mrefu kuvamia USSR?

Adolf Hitler mara kwa mara alibadilisha mtazamo wake kuhusu mambo makubwa, lakini nadhani uvamizi wake wa USSR ni jambo ambalo lilianza mwisho mwisho wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Chuki yake dhidi ya utawala wa kikoministi ulikuwa mbaya sana, lakini wazo hilo pia liliathiriwa na uvamizi wa Wajerumani wa Ukraine mnamo 1918 na imani kwamba inaweza kuwa tunu njema siku zijazo.

Kukomboa eneo hilo kungelizuia kurejelewa kwa kizuizi cha Uingereza na njaa iliyoshuhudiwa Ujerumani kufutia Vita vya Kwanza vya Dunia. Kwa hivyo ilikuwa hatua ya kimkakati.

Ulinzi dhidi ya uvamizi wa Wajerumani ulihamasisha jamii nzima. Katika picha hii baadhi ya wanawake wanaonekana wakifanya kazi latika kiwanda cha majeshi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Ulinzi dhidi ya uvamizi wa Wajerumani ulihamasisha jamii nzima. Katika picha hii baadhi ya wanawake wanaonekana wakifanya kazi latika kiwanda cha majeshi

Kinadharia mpango ulikua ni kuendelea na oparesheni hiyo hadi Disemba mwaka 1940. Cha kufurahisha ni kwamba, Hitler alihalalisha uvamizi wa USSR kwa majenerali wake kama njia pekee ya kuiondoa Uingereza vitani.

2. Je! Makubaliano ya Wajerumani na Sovieti yalikuwa zaidi ya suluhisho la muda kwa Hitler?

Ilikuwa hatua ya muhimu kwa lengo maalum. Hitler alielewa kwamba ni alzima ashinde washirika wa Magharibi.

Na hii inaonyesha ujasiri wa kushangaza, haswa ikizingatiwa kuwa jeshi la Ufaransa lilikuwa na nguvu zaidi wakati huo.

Makubaliano na Ribbentrop-Molotov, kati ya Wanazi na Wasovieti “yaliifanya nusu ya Ulaya kutaabika kwa miongo kadhaa”

Stalin, kwa upande wake, alikuwa na matumaini makubwa kwamba majimbo ya kibepari na Wanazi wataangaizana.

Makubaliano ya Ujerumani -Sovieti yalikuwa muhimu kwake pia kwasababu, kwa sababu alikuwa amevunja jeshi la (Red Amy) na alihitaji kuahirisha makabiliano yoyote na Ujerumani.

3. Ujerumani imekuwa ikikosolewa kwa kusubiri kwa muda mrefu kufanya uvamizi huo. Unakubaliana na hili?

Bila shaka, ni kweli kwamba oparesheni ya Barbarossa ilichelewa sana na kumekuwa na mjadala kwanini ilichelewa hivyo. Nadharia ya zamani inadai kwamba ilikuwa uvamizi wa Ugiriki mnamo Aprili 1941 ambao ulifanya iahirishwe, lakini tayari wakati huo ilijulikana kuwa sababu kuu ilikuwa muda.

Msimu wa baridi kali wa mwaka 1940-1941 ulikumbwa na mvua hali ambayo ilisababisha matatizo mawili. Kwanza, uwanja wa ndege wa Luftwaffe, uliotumiwana jeshi la anga la Ujerumani, ulikuwa imesombwa na maji na haukuweza kabisi kupokea ndege.

Joachim von Ribbentrop (kushoto), Stalin na Viacheslav Molotov (wa kwanza kulia) wakati wa kutiwa saini makubaliano ya Agosti 23, 1939.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Joachim von Ribbentrop (kushoto), Stalin na Viacheslav Molotov (wa kwanza kulia) wakati wa kutiwa saini makubaliano ya Agosti 23, 1939.

Pili, hali mbaya ya hewa ilichelewesha kupelekwa kwa uchukuzi wa magari katika ngome ya mashariki.

Jambo lingine la kufurahisha ni kwamba karibu 80% ya huduma ya usafirishaji wa magari ya Ujerumani ulitoka kwa jeshi la Ufaransa iliyoshindwa.

Ndio sababu kwanini Stalin aliikosoa vikali Ufaransa katika kongamano la Tehran la mwaka 1943 akisema kuwa inastahili kuchukuliwa kama wasaliti. Ukweli kwamba hawakuharibu magari yao wakati walipojisalimisha, kwa Stalin ilikuwa hatua mbaya sana dhidi yake.

4. Inajulikana kuwa Stalin alikuwa mwangalifu sana. Angewezaje kupuuza ishara kadhaa juu ya shambulio la Wajerumani?

Hii ni moja ya kitendawili kikubwa katika historia.Stalin, mmoja wa wanaume wenye tuhuma alihadaiwa na Hitler.Ilichangia nadhari kadhaa kwamba Stalin alikuwa anapanga kuvamia Ujerumani kwanza.

German troops advance in Ukraine. Their advance would slow down later.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Vikosi vya Ujerumani vikielekea Ukraine. Baadaye walipunguza kasi ya mashambulizi

Hata hivyo nadharia hiyo owever, that theory doesn’t make much sense.Inaegemea mpango wa dharura wa Sovieti uliobuniwa Mei 11, 1941 ambapo Jenerali Zhukov na wengine, walijua kuhusu mpango wa uvamizi wa Wanazi na tathmini ya jinsi ya kujibu mashambulizi.Moja ya wazo walilokuwa nalo ni kuvunja shambulio kabla halijafanyika.Lakini Red Army haikuwa na uwezo wa kuchukuahatua kama hiyo.Hii ni kwa sababu uchukuzi mkuu wa silaha zake ulikuwa ni trakta ambazo zilikuwa zikitumiwa kulimia!

Soviet soldiers stack objects captured from their German enemies in Murmansk, Russia.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Moja ya wazo walilokuwa nalo ni kuvunja shambulio kabla halijafanyika.

Lakini cha kufurahisha zaidi ni jinsi Stalin alivyopuuza ishara zote alizopokea.Sio kutokakwa Uinhereza pekee bali pia kutoka kwa wanadiplomasia wao wenyewe na majasusi.

Pengine huenda hatua hiyo inaelezea msimamo wake tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uhispania ambapo alijiridhisha watu wotee wanaoishi ughaibuni ni wafisadi na hawakuupenda muungano wa Sovieti.

Hii ndio sababu hakutilia maanani kilichoendelea Berlin, hata vbaada ya kutumiwa kamusi ndogo ya wanajeshi wa Ujerumani iliyojumuisha maelezo kama vile “nipeleke katika shamba lako la kijamii.” Alidhani yote ni uchokozi wa Uingereza kulazimisha vita dhidi ya Ujerumani.

5. Lengo la Ujerumani lilikuwa lipi? Je kweli walikuwa na mpango wa kuteka kabisa USSR?

Mpango ulikuwa kufika sehemu iliyojulikana kama mstari wa AA line, kutoka Archangel hadi Astrakhan. Hii ingelewapeleka hadi Moscow na kusonga mbele zaidi ya Volga.

Kwa hivyo wakati vita vya Stalingrad vilipoanza, baadhi ya wanajeshi wa Ujerumani waliamni kwa kuteka mji mmoja na kufika Volga watakuwa wameshinda vita.

The long Nazi siege of Stalingrad was one of the bloodiest battles of the entire war. In the picture, Soviet snipers in a defensive position.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Mashambulio ya muda mrefu ya Wanazi katika eneo la Stalingrad yalikumbwa na umwagikaji mkubwa wa damu kipindi chote cha vita.

Waliamini wanajeshi wa Sovieti walioponea mapigano makali mwanzoni mwa vita hawatakuwa na nguvu ya kuhimili makombora kutoka angani.

Pia walikuwa na wzo la kuanzisha makazi ya Wajerumani katika maeneo waliyoteka Urusi na Ukraine. Kulingana na mkakati wa njaa wa Ujerumani watu wanaoishi katika miji mikubwa wangelikuwa wamelemewa na njaa na kufa. Inakadiriwa watu milioni 35 walifariki.

Mpango huo wote ulitegemea kufika kwao katika eneo la AA, na zidi ya yote kuvunjwa kwa Red Army baada ya kuzingirwa kwa muda mrefu.

6. Je, Wjerumani walikuwa na nafasi ya ushindi?

Kufikia mwishoni mwa mwaka 1941, katika hali ya taharuki, Stalin alimwambia balozi wa Bulgaria kuwa anadhani Moscow inaweza kuangukia katika mikono ya adui na anahofia kila kitu kitaparaganyika.

Lakini balozi Stamenov, akajibu: “Huyu ni mwehu. Hata akikimbilia katika milima ya Ural, bado atashinda vita.”

Jibu hilo linathibitisha ni kwa nini ilikuwa vigumu kwa Operesheni Barbarossa kufanikiwa. Ukubwa wa Urusi ulimaanisha kuwa Wehrmacht na vikosi vinavyomuunga mkono kutoka Romania na Hungary hawakuwa na wanajeshi wa kutosha wa kuikamata nchi nzima.

The 1,000-year Reich that Hitler promised came to an end after 12 years.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Pili, Hitler hakujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na Japani kwa kuivamia Uchina. Japani pia ilikuwa na jeshi imara lenye vifaa vya teknolojia ya juu. Jeshi hilo likalivamia taifa kubwa la China.

Somo hapa ni kuwa, mwanzoni mwa operesheni, dalili za ushindi huchomoza, lakini mtikisiko wa hofu na ukatili (ambao pia Hitler aliufanya kwa Wasovieti) mwishowe huzaa upinzani mkali na ghasia kubwa.

Hitler hakuliona hilo kabisa. Yeye aliamini katika falsafa yake kuwa; “Vunja mlango na jengo zima litaporomoka,” akadharau kabisa uzalendo mkubwa wa raia wa Usovieti ambao walipigana mpaka dakika ya mwisho na kumshinda.

7. Je, ni sahihi kusema Stalin alikuwa kikwazo kwa mfumo wa kujihami wa Usovieti?

Kukataa kwake kuruhusu vikosi kurudi nyuma, hususani baada ya kuzingirwa kwa jiji la Kiev kulisababisha maelfu ya wana kesho kupoteza maisha. Ilikuwa ni amri ambayo haikuwa na chaguo zuri, aidha uikatae ama ufe.

Stalin alilegeza kamba kwa kuchelewa na kuruhusu vikosi chake kurejea Moscow, uamuzi ambao ulikuwa na tija kwa kuwa uliokoa wanajeshi wengi ambao baadae waliuokoa mji mkuu wao usitekwe na adui.

8. Je kulikuwa na hatari ya utawala wa Usovieti kuanguka mwanzoni mwa uvamizi?

Hapakuwa na uwezekano wa watu kuandamana ili kumng’oa Stalin madarakani.

Pia wala hakukuwa na wengi ambao walimkosoa, kwa kuwa wengi wao hawakujua nini kilikuwa kinaendelea na hasira yao ilikuwa kwa Wajerumani ambao wamevunja mkataba wa amani na nchi yao.

Stalin hakukumbwa na hatari ya kupinduliwa.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Stalin hakukumbwa na hatari ya kupinduliwa.

Stalin mwenyewe alihofia zaidi kupinduliwa na wasidizi wake. Wakati fulani akiwa ameenda mapumziko huku akiwa amechanganyikiwa kabisa alitembelewa na wasaidizi wake akadhani wameenda kumkamata.

Hata hivyo akagundua kuwa wasidizi hao walikuwa wameingiwa na woga kama yeye na wakamshawishi arejee kutoka mapumzikoni ili kuwaongoza.

9. Je, baridi kali la Urusi liliamua mshindi wa mapambano ya Moscow?

Hakuna shaka kuwa baridi kali lilikuwa ni jambo muhimu sana katika mapambano hayo.

Ilikuwa ni baridi kali kweli kweli, huku nyuzi joto zikianguka mpaka kufikia -40. Hili ni baridi kali zaidi ya hata ya kwenye jokofu (friji) na Wajerumani hawakuwa wamejiandaa ipasavyo kukabiliana nalo kisilaha na mavazi.

Bunduki za Wajerumani mathalani mara kwa mara ziliganda na kuwalazimu kuzikojolea ili kuzipa joto.

Vifaru vya Ujerumani vilikuwa na matairi myembamba hivyo havikufua dafu kwenye theluji, wakati huo huo vifaru vya Usovieti vikitamba.

Ukali wa baridi ulitatiza uvamizi wa jeshi liloogopwa la askari wa miguu wa Ujerumani.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Ukali wa baridi ulitatiza uvamizi wa jeshi liloogopwa la askari wa miguu wa Ujerumani.

10Je, kuivamia USSR ndio kosa kubwa kuwahi kufanywa na Hitler?

Bila ya shaka.

Laiti kama Hitler angelikubaliana na hali halisi baada ya kushindwa nchini Ufaransa na kisha kuliboresha jeshi lake kwa rasilimali za nchi ambazo alishazipiga, Ujerumani ingekuwa nguvu kubwa baada ya muda mfupi.

Hivyo, laiti Stalin angelijaribu kuishambulia kwanza Ujerumani baina ya 1942 na 1943 basi Umoja wa Usovieti ungelijichimbia kaburi.

Lakini, kitendo cha Hitler kuishambulia Usovieti kilibadili kila kitu, ni operesheni Barbuda ambayo ilivunja uti wa mgongo wa jeshi la Ujerumani.