Na Mathew Kwembe, Mtwara
Timu ya soka ya wavulana ya Mkoa wa Kagera imefufua matumaini yake ya kufanya vizuri katika michuano ya UMISSETA inayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu na Shule ya Ufundi Mtwara baada ya kuichapa Pwani magoli 2-1.
Huu ni mchezo wa pili kwa Kagera baada ya kufungwa katika mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya bingwa Mtetezi wa kombe hilo timu ya mkoa wa Geita baada ya kuchapwa goli 1-0.
Katika mchezo wa jana magoli ya Kagera yalifungwa katika kipindi cha kwanza na washambuliaji Vasco Mkande na Dikson Boniface.
Mara baada ya mchezo huo Kocha wa Kagera Hashim Mwakawago ambaye anafundisha shule ya sekondari ya Rugambwa mkoani Kagera alisema kuwa wachezaji wake walijituma kwa bidii kuupata ushindi huo.
Mwakawago amesema timu yake itajitahidi kufanya vizuri ili isonge mbele katika michezo inayofuata ambapo leo atacheza na Mbeya na kufuatiwa na michezo mingine dhidi ya Ruvuma, Tabora na kumaliza na Kilimanjaro katika hatua ya makundi.
Matokeo ya michezo mingine kwa upande wa soka wavulana Njombe imefungwa na Tanga magoli 3-0,Rukwa imeichapa Iringa 1-0, nayo Tabora imeifunga Mbeya 1-0, Kigoma imefungwa na Simiyu magoli 1-2 huku Dar es salaam na Lindi zikitoka sare ya 1-1.
Matokeo mengine ya soka wavulana Manyara imeifunga Shinyanga 1-0, Mabingwa watetezi Geita nao wamechapwa na timu machachari ya Ruvuma 0-1, Dodoma na Katavi zimetoka suluhu na Songwe imeichapa Pemba 1-0.
Katika mchezo wa soka wasichana Singida imeifunga Geita 1-0, Mwanza imechapwa na Tabora 1-2, Mtwara nayo imefungwa na Mwanza 0-3, Manyara imeifunga Songwe 3-0, Arusha imeifunga Dodoma 1-0, Mbeya imechapwa na Morogoro 1-2, Kagera na Kilimanjaro zimetoka sare 1-1, Ruvuma nayo imetoka sare na Dar es salaam magoli 3-3 na Dar es salaam imeifunga Simiyu magoli 2-1.
Kwa mchezo wa mpira wa mikono handball wavulana Lindi dhidi Simiyu 19-16, Kilimanjaro dhidi ya Geita 13-25, Dar es salaam dhidi ya Mara 17-22, Iringa dhidi ya Ruvuma 7-9, Arusha dhidi Ruvuma 39-26, Pwani dhidi ya Njombe 36-14, Shinyanga dhidi ya Tanga 8-31 na Manyara dhidi ya Dodoma 20-22.
Mpira wa mikono wasichana Mwanza imefungwa na Tanga kwa magoli 11-19 na Lindi dhidi Morogoro 4-17.
Kwa upande wa mchezo wa Netiboli Mara 32 dhidi ya 19 Arusha, Kagera 25 dhidi ya Lindi 12, Manyara 20 Pwani 31, Dar es salaam 37 dhidi ya Ruvuma 9, Geita 18 dhidi Songwe 32, Mtwara 15 dhidi ya Rukwa 34, Unguja 12 dhidi ya Singida 29, Iringa 16 dhidi ya Dodoma 18, Kilimanjaro 22 dhidi Tanga 23.
Pia Shinyanga 30 dhidi Katavi 20, Tabora 38 dhidi Simiyu 11 na Arusha 22 dhidi Njombe 12.
Matokeo ya mpira wa wavu wavulana Mtwara imeifunga Tabora seti 3-2, Mbeya imeifunga Kagera seti 3-0, Mara imeichapa Pemba seti 3-0, Arusha imeichapa Iringa 3-1, na Tanga imefungwa na Dodom,a kwa seti 1-3, Rukwa imeifunga Kigoma seti 3-0.
Michezo mingine imeshuhudia Manyara ikipoteza kwa mwanza seti 1-3, Ruvuma nayo ikipoteza kwa Arusha seti 3-0, Shinyanga ilifungwa na Dodoma kwa seti 2-3, Lindi nayo imefungwa na Kigoma seti 3-0, Simiyu imefungwa na Mwanza seti 1-3 na Kilimanjaro imeifunga Tanga seti 3-0.
Katika mpira wa wavu wasichana Kigoma imechalazwa na Tanga seti 0-3, Mara dhidi ya Kilimanjaro seti 3-0, Mtwara dhidi ya Arusha 3-0 na Dar es salaam dhidi ya Iringa seti 3-0.
Katika mpira wa kikapu wavulana Geita ilichabangwa na Geita 54-45, Mwanza dhidi ya Kigoma 66-15, Mtwara dhidi ya Kilimanjaro magoli 11-47, Ruvuma dhidi ya Pwani 18-46, Morogoro dhidi ya Iringa 97-39, Lindi dhidi ya Njombe 11-15, Arusha dhidi ya Simiyu 44-33 na Songw dhidi ya Mbeya 13-33.
Katika mpira wa kikapu wasichana Shinyanga imeifunga Mtwara magoli 20-10, Geita dhidi ya Lindi 27-19, Iringa dhidi ya Mwanza 6-87, Kilimanjaro dhidi ya Arusha 18-44 na Dodoma dhidi ya Simiyu.
Michuano hiyo itaendelea hapo leo katika viwanja mbalimbali vya Chuo cha Ualimu na Shule ya Ufundi Mtwara