Friday, November 15

VIDEO: NGO’s kuweka alama za kimaendeleo katika jamii pale wanapotekeleza miradi yao.

 

Na Raya Ahmada.-PEMBA.

 

Mrajis wa Jumuiya Zisizo za Kiserikali Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla amesema wakati umefika kwa jumuiya za kiraia kuweka alama za kimaendeleo katika jamii pale wanapotekeleza miradi mbali mbali wanayoiyomba kwa wafadhili wa maendeleo.

 

Kauli hiyo ameitowa ukumbi wa Jamuhuri Wete kwenye uzinduzi wa mradi wa kuongeza uwajibikaji na uwazi katika maamuzi kwenye halmashauri pamoja na matumizi ya rasilimali za umma unaotekelza na jumuiya ya PEPOHUDA, uliowashirikisha masheha wa shehia kumi na mbili pamoja na waratibu wa wanawake na watoto, na kuwataka wadau hao kuwa mstari wa mbele ili kuona mipango ya maendeleo katika serikali za mitaa inamuhisha vipi mtoto wa kike.

 

Mapema akielezea lengo la mradi huo Mratibu wa jumuiya ya kupunguza umaskini na kuzidisha maendeleo ya watu PEPOHUDA Said Mbarouk Juma amesema ni kuwawezesha watoto wa kike kushiriki katika mipango ya maendeleo katika serikali za mitaa ili sauti zao zisikike na mahitajio yazingatiwe.

 

Wakielezea matarajio yao wadau wa mradi huo walikuwa na haya ya kusema

Mratibu wa jumuiya zisizo za kiserikali ofisi ya Pemba Ashraki Hamad Ali ameiyomba jumuiya ya PEPOHUDA kuendelea kuomba miradi mbali mbali kulingagana na matatizo yanayowakabili wananchi

 

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI