Wednesday, January 15

Mawaziri wa Elimu na Fedha wa Zanzibar Waendelea na Ziara Yao Nchini Uturuki.

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Uturuki HAYDARPASA MESLEKI ve TEKNIK ANADOLU LISESI wakiangalia mafunzo mbali mbali ya Amali yanayotolewa chuoni hapo,.katikati ni waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali mhe Simai Mohammed Said na wa kwanza kulia waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na.Mipango Mhe Jamal Kassim Ali.

 

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Uturuki HAYDARPASA MESLEKI ve TEKNIK ANADOLU LISESI wakiangalia mafunzo mbali mbali ya Amali yanayotolewa chuoni hapo.

Na Maulid Yussuf WEMA. UTURUKI.
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaendelea na ziara yao nchini Uturuki kwa kuonana na Shirikisho  huru la wenye Viwanda na Wafanyabiashara wa Istanbul MUSIAD.
Katika mazungumzo yao, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha.na.Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali amewaelezea kuwa Zanzibar imefungua mipaka ya kupokea wawekezaji kutoka nje kupitia utaratibu wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Serikali na Mashirika binafsi yaani Public Private Pertnership (PPP).
Pia Mhe. Jamal amelielezea Shirikisho hilo kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeweka miradi ya kimkakati kwa ajili ya kufanya Mapinduzi ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Mafuta na Gesi pamoja na ujenzi wa Viwanja vya Ndege.
Aidha Mhe. Jamal amewaalika wawekezaji kutoka Uturuki na kuwaahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji Zanzibar.
Nae Mwenyekiti wa Shirikisho huru la wenye viwanda na Wafanya biashara Mr. ZEKI GUVERCIN amewataka Mawaziri hao kutuma taarifa muhimu kwao  zinazohusu maeneo ya uwekezaji ya Zanzibar pamoja na namna mazingira rafiki ya uwekezaji ili wafanye maamuzi sahihi.
Pia ameelezea kuwa wapo tayari kutoa mashirikiano katika masuala ya biashara pamoja kwamba wapo  tayari  kuwaunganisha na Makampuni maarufu ya Wafanya biashara ambayo yana nia ya kufanya biashara na uwekezaji katika maeneo ya kimkakati ya uwekezaji Zanzibar.
Wakati huo huo Mawaziri hao wametembelea Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Uturuki HAYDAR PASA MESLEKI ve TEKNIK ANADOLU LISESI na kukubaliana kufanya uwezekano wa kubadilishana Wanafunzi kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Amali kati ya Zanzibar na Uturuki.