Thursday, January 16

ZAIDI YA MIAKA 30 ILIYOPITA, HAWA HAPA NDIO WALOONGOZA SOKA LA ZANZIBAR, WOTE WAMEJIUZULU WENYEWE

Na aAbubakar kisandu  -Zanzibar.
Unapolizungumzia Soka la Zanzibar hutoacha kumtaja Marehemu Ali Ferej Tamim aliyeongoza Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) kwa zaidi ya miaka 20 mpaka pale June 30, 2012 kujiuzulu nafasi yake ya Urais.
ZFA kwasasa inatambuliwa kama ni ZFF, ilitoka kwenye Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na tangu June 2 ,2019 kuwa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF).
WAJUWE BAADHI MARAIS WA ZFA/ZFF
June 30, 2012 Amani Ibrahim Makungu (pichani) alishinda Urais wa ZFA baada ya kupata kura 49 zilizomkubali na kura 3 zilimkataa kati ya kura 52 zilizopigwa kwenye Uchaguzi huo ambao mgombea alikuwa pekee, aliipokea nafasi hiyo kutoka kwa Fereji aliyeongoza ZFA zaidi ya miaka 20.
Makungu aliongoza ZFA kwa takribani miezi 8 tu baada ya Machi 4, 2013 kujiuzulu nafasi yake.
June 8, 2013 Ravia Idarous Faina akafanikiwa kushinda Urais wa ZFA baada ya kupata kura 37 huku mpinzani wake mkubwa Abdallah Juma Mohammed alipata kura 16 ambapo Rajab Ali Rajab hakupata kura hata moja.
April 14, 2016 Ravia akashinda tena Urais wa ZFA kufuatia kupata kura 47 na kumshinda Salum Nassor Bausi aliyeambulia kura 6 tu kati ya kura 53 zilizopigwa.
June 6, 2018 Ravia akajiuzulu nafas yake ya urais ndani ya ZFA.
June 2, 2019 Seif Kombo Pandu alifanikiwa kuwa Rais wa ZFF baada ya kupata kura 16, akiwashinda Khamis Abdallah Said aliyepata kura 7 na Ame Abdallah Dunia aliyeambulia kura 5 kati ya kura 28 zilizopigwa.
February 17, 2021 Pandu akajiuzulu nafasi yake hiyo ya Urais ndani ya ZFF na kupelekea June 27, 2021 kufanyika Uchaguzi wa kumtafuta Rais mpya wa ZFF.
HISTORIA inaonyesha karibu ya Marais wote hao wametoka madarakani baada ya wao wenyewe kujiuzulu na sio kushindwa katika Uchaguzi, mfano Marehemu Ali Ferej Tamim alijiuzulu mwenyewe, akaongoza Amani Ibrahim Makungu Miezi 8 tu akakaa pembeni mwenyewe, akaja Ravia Idarous Faina nae akaongoza baadae mwenyewe kajiuzulu, akafuatia Seif Kombo Pandu kaongoza hata miaka 2 hajafika nae kajiuzulu, kunani ZFF?
Sasa tunasubiri June 27, 2021 kumjuwa nani atashinda Urais kati ya Wagombea 5 waliopitishwa Abdul-latif Ali Yassin, Abdul- kadir Mohamed Abdul-kadir (Tashi), Haji Sheha Hamad, Suleiman Shaaban Suleiman na Suleiman Mahmoud Jabir ?.