NA ZUHURA JUMA, PEMBA.
JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamshikilia mkaazi wa shehia ya Kifundi wilaya ya Micheweni kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka miwili (2).
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 anadaiwa kutekeleza tukio hilo la kinyama siku ya tarehe 24 mwezi huu majira ya saa 1:00 usiku.
Taarifa ambazo zimepetikana zinasema kwamba mwathirka wa tukio hilo anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Micheweni.
Mmoja wa wanafamilia wa ya mtoto huyo, amesema kwamba mtoto huyo ameshonwa nyuzi tatu sehemu zake za siri baada ya kupata athari wakati akifanyiwa kitendo hicho cha kikatili.
“Kwa sasa tupo hospitali ya Micheweni tumelazwa na mtoto ameshonwa nyuzi tatu sehemu zake za siri, kwani alikuwa amemchana hasa sehemu za nyuma”, alieleza mwanafamilia hiyo.
Sheha wa Shehia ya Kifundi Mariam Mjawiri akizungumzia tukio hilo alisema, ni kweli limetokea katika shehia yake na kusema tayari mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Juma Sadi Khamis amethbitisha tukio hilo na kusema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
“Ni Kweli kuna tukio na ubakaji limetokea katika shehia ya Kifundi Konde Wilaya ya Micheweni, ambapo mtuhumiwa huyo wa miaka 16 tunashikilia na anasubiri upelelezi ukamilike ili afikishwe mahakamani”, alisema Kamanda Sadi.
Aidha Kamanda Sadi aliishauri Mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wa matendo ya udhalilishaji, kwani inaweza kuwa fundisho na mwarubaini wa matendo hayo.
“Mahakama inafanya kazi nzuri ya kuwatia hatiani wahusika wa matendo hayo, lakini inawezekana adhabu ya miaka saba au chini yake haijaweza kukomesha”, alishauri.
Hata bivyo baadhi ya wananchi wa kijiji cha Matangatuani shehia ya Kifundi waliishauri taasisi husika kufanya uchunguzi kwa kina juu ya umri wa mtuhumiwa, kwani umri wake ni zaidi ya miaka 16.