Tuesday, November 26

AirCar: Gari linalopaa angani lafanikiwa kuruka kutoka uwanja mmoja wa ndege hadi mwengine

Gari la mfano linaloweza kupaa angani limekamilisha dakika 35 angani kati ya viwanja vya ndege huko Nitra, na Bratislava nchini Slovakia.

Gari hilo kwa jina ‘Aircar'{Gari ndege} lina injini ya gari la BMW na hutumia mafuta ya petroli.

Muundaji wake Profesa Stefan Klein , anasema kwamba linaweza kupaa angani kwa zaidi ya kilomita 1000 na urefu wa juu wa futi 8,200 na kufikia sasa limefanikiwa kukaa angani kwa saa 40.

Inachukua dakika mbili na sekunde 15 kubadilika kutoka kuwa gari hadi ndege.

‘linapendeza’

Mbawa zake nyembamba hujikunja kando kando ya gari hilo.

Profesa Klein aliiendesha katika barabara ya ndege hadi mjini alipowasili , akitazamwa na waandishi wa habari walioalikwa.

Alielezea uzoefu huo mapema siku ya Jumatatu kama wa kawaida na wa kupendeza.

Likiwa angani gari hilo lilikuwa na kasi ya kilomita 170 kwa saa. Linaweza kubeba watu wawili, wakiwa na uzito wa kilo 200.

Lakini likilinganishwa na ndege zisizo na rubani inaweza kupaa wima na inahitaji barabara ya ndege.

AirCar in flight

CHANZO CHA PICHA,KLEIN VISION

AirCar outside airport

CHANZO CHA PICHA,KLEIN VISION

Mwaka 2019, kampuni ya Morgan Stanley ilitabiri kwamba sekta hiyo huenda ikawa na thamani ya $1.5trillion (£1tn) kufikia 204

Na katika sherehe ya magari siku ya Jumanne , afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Hyundai Motors Michael Cole aliutaja mpango huo kama mpango wa siku za usoni.

Unaonekana kama suluhu mwafaka ya mkazo uliopo katika miundo mbinu ya uchukuzi iliopo.

‘Soko kuu’

Kampuni iliotengeneza ‘Garindege’ hilo , Klein Vision inasema kwamba mfano huo umechukua takriban miaka miwili kutengeneza na gharama yake ni chini ya £1.7m katika uwekezaji.

Anton Rajac, mshauri na mwekezaji katika kampuni ya Klein Vision , alisema iwapo kampuni hiyo itavutia asilimia ndogo ya wawekezaji wa ndege ama mauzo ya teksi utafanikiwa pakubwa.

”Kuna takriban maagizo 40,000 ya ndege nchini Marekani pekee”, alisema.

”Na iwapo tutabadilisha asilimia 5 kati yazo, kubadilisha ndege na badala yake kununua magari yanayo paa , tuna soko kubwa”.

‘Kitu kizuri sana’

Dkt Stephen Wright, mtafiti mwandamizi wa mashine za ndege katika chuo kikuu cha West of England , alielezea AirCar kuwa mtoto wa gari aina ya Bugatti Veyron na Cesna 172. “.

Na hakufikiria kwamba gari hilo litakuwa na matumizi ya kiwango cha juu cha bei ya mafuta ikilinganishwa na ndege nyengine.

”Lazima nikiri kwamba hii inakaa vizuri sana – lakini nina maswali 100 kuhusu cheti”, alisema Dkt Wright.

”Mtu yeyote anaweza kutengeneza ndege lakini ujanja ni kutengeneza ndege inayoweza kuruka kwa saa milioni, huku ikiwa na mtu ndani yake na bila kusababisha ajali yoyote”.

”Nasubiri kuona nakala ambayo itasoma , hii ni salama kupaa angani na salama kuuza”.0.