Monday, November 25

VIDEO: Presha ya ujauzito ni chanzo cha vifo vya kina mama na watoto fika kituo cha afya mapema pindi ukiona dalili za ujauzito.

NA KHADIJA KOMBO. PEMBA.                                                                                                

Imeelezwa kuwa vifo ving ivya  mama wajawazito na watoto vinatokana na presha ya mimba hivyo ni vyema kwa akina mama mara wanapojihisi kuwa wajawazito kukimbilia vituo vya afya ili kupata ushauri zaidi.

Mkuu wa kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza kutoka Hospitali kuu ya mnazi mmoja Dr.Ummukulthum Omar Hamad ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa mada kwa wahudumu wa Afya katika ngazi ya jamii huko katika ukumbi wa Samail Gombani Pemba.

Amesema kutokana na hali hio ni vyema kwa wahudumu hao kuishajihisha jamii juu ya akina mama kwenda kituo  cha afya mapema mara tu wanapojibaini na dalili za ujauzito kwa lengo la kuchunguzwa afya zao, kitu ambacho kitasaidia kubaini taizo mapema na kulipatia ufumbuzi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Utafiti Dr Omar Mwalim Omar amesema kutokana na utafiti walioufanya kwa upande wa tatizo la presha kwa mama wajawazito wamegundua kwamba ni kubwa na kuna baadhi ya vituo hawafanyiwi vipimo kama inavyostahiki.

Akizungumzia kuhusu lengo la mafunzo hayo Dr. Zuhura Saleh Amour kutoka katika kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza Zanzibar amesema ni kutaka kuwasilisha ripoti juu ya utafiti walioufanya juu ya afya za akina mama wenye ujauzito hasa katika maradhi ya presha za wajawazito.

Hivyo amewataka wahudumu hao kuwa makini katika kutoa huduma stahiki kwa mama  hao ili kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyodhaminiwa na Costech yaliwashirikisha Wahudumu wa afya ngazi ya jamii, wanajamii pamoja na watoa huduma ya kwanza red cross.

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI