NA KHADIJA KOMBO -PEMBA
Walimu wa Skuli za Msingi na Sekondari Kisiwani Pemba, wameshauriwa kujifunza taaluma ya kutumia maitandao ili kurahisisha ufundishaji kwa wanafunzi Maskulini.
Ushauri huo umetolewa na Raisi wa Jumuiya ya Shaib Foundation, Mustafa Moyo katika mafunzo ya matumizi ya mitandao yaliyoshirikisha walimu wa Skuli mbalimbali za Msingi na Sekondari Kisiwani Pemba, mafunzo yaliyofanyika Maktaba kuu ChakeChake
Amesema Walimu wanapaswa kutumia mitandao kwa lengo la kuendana na wakati wa mabadiliko ya teknolojia. Hivyo jumuiya hio imetoa mafunzo hayo kwa walimu kutoka sukuli mbali mbali kisiwani Pemba,
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yataweza kuwasadia kwa kiasi kikubwa katika ufudishaji wa wanafunzi maskulini.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI