ABDI SULEIMAN.
MWAKILISHI wa Jimbo la Ole Massoud Ali Mohammed, amesema lengo la kukabidhi bati 20 zenye thamani ya shilingi laki 388,000/= kwa madrasat-Nur Muhammadia, ni hatua za mwanzo za kuboresha madrasa hiyo ili kuweza kuwa ya kisasa zaidi.
Alisema ili wanafunzi waaweze kusoma kwa bidii na kupata mafanikio, wanahitaji kuwa katika mazingira mazur hivyo kujengewa kwa madrasayo itakuwa ni moja ya sehemu itakayowafanya wasome bila ya hofu.
Akizungumza na walimu, wazazi na wanafunzi wa madrasa hiyo, katika kijiji cha Gongoni Uwandani Wilaya ya Chake Chake, Afisa mdhamini Wizara ya nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Pemba Thabit Othaman Abdalla, kwa niaba ya Mwakilishi wa Jimbo hilo.
Alisema kukamilika kwa ujenzi wa madrasa hiyo, wanafunbzi wataweza kusoma katika mazingira mazuri na kupata elimu bora ya dini.
“Sisi hapa tumekuja kwa ajili ya kukabidhi bati hizi 20, msaada huu umetolewa na mwakilishi wenu ambaye ni waziri katika serikali hii, inayoongozwa na Rais Dk. Miwnyi, katika kusaidia hili hakubagua chama wala nini ametoa kwa ajili ya dini”alisema.
Hata hivyo Mdhamini Thabiti, aliwataka wazazi, walezi na wanafunzi wa madrasa hiyoi kuendelea kuwaombea dua viongozi wa nchi, ili kufikia malengo yao waliojiweka katika kuibadilisha Zanzibar.
Naye mwalimu wa madrasa hiyo maalim Ali Kombo, alisema bati hizo zitaweza kuwasaidia kwa hatua ya kwanza, kwa kuhakikisha wanazipachika na kuondosha tatizo la kuvuja kwa chuo hicho kipindi cha mvua.
Alisema licha ya chuo hicho kuvuja hulazimika watoto kuwakusanya katika banda moja na kuendelea na masomo, jambo ambalo Mwakilishi wa jimbo la ole sasa amewaunga mkono.
Akizungumzia mikakati yao alisema ni kuhakimkisha wanajenga madrasa ya kisasa, ambayo itaweza kusomesha wanafunzi wengi kwani sehemu hiyo wanayo.
Hata hivyo aliwaomba wadau wengine kujitokeza kwa hali na mali, kuunga mkono juhudi za kuwasaidia katika masuala ya dini ili kuweza kuendeleza elimu katika kijiji chao.
“Hebu tizama hivi kilivyo chuo kinawanafunzi 160, hii sehemu sasa imeshakua ndogo inahitajika sehemu kubwa ili wanafunzi wapate kusoma kwa utulivu”alisema.
Kwa upande wake mdau wa elimu katika kijiji cha Uwandani Kombo Ali alisema sasa wanafunzi wataweza kusoma kwa amani na kufikia mafanikio yao, kwani hapo awali walikuwa wakilazimika wakati wa mvua kuchanganywa upande mmoja.