NA ABDI SULEIMAN.
IKIWA serikali ya SMT na SMZ, zimeanza kuchukua juhudi za kukabiliana na wimbo la tatu la maradhi ya Covid 19, halitame viongozi wa serikali Kisiwani Pemba, wamesema kuwa tayari mikakati mbali mbali imeshaanza kuchukulia katika kukabiliana na wimbi hilo.
Viongozi hao wamesema tayari mikakati mbali mbali wameshaanza kuipanga, katika kukabiliana na wimbo hilo ikiwemo kuimarisha huduma katika maeneo yote yenye mikusanyiko ya jamii.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tafauti kwa njia ya simu, wamesema kuwa moja ya mikakati hiyo ni kusambaza kwa vifaa vya kunawiya mikono katika maeneo hayo.
Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, alisema miongoni mwa mikakati ambayo wameanza kuichukua ni kuwapatia elimu wananchi juu ya kujikinga na wimbo la tatu la Covid 19, inayoendelea duniani na barani Afrika.
“Tumeanza na vitakasa mikono, ndoo zenye maji ya kutiririka, kuweka katika maeneo yenye watu wengi, ikiwemo sokoni, stendi za gari hata katika hospitali zetu, lengo ni kudhibiti maambukizi ya janga la Covid 19”alisema.
Aidha aliwataka wananchi kutokudharau au kupuuza maelekezo yote wanayopatiwa na serikali, pamoja na wataalamu wa afya katika kujikinga na ugonjwa huo.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwashauri wananchi wanapohitaji huduma za afya, kutumia vituo vilivyokaribu navyo kwa lengo la kuepusha msongamano wa watu kwenye hospitali za Wilaya.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, alisema wanatarajia kukutana hivi karibuni na watendaji wa wizara ya afya, kwa ajili kuona hatua na mikakati watakayoichukua katika kukabiliana na wimbi la janga la Covidi 19.
“Maagizo na mikakati yoyote yatakayotolewa na wataalamu wetu wa afya, inapaswa kutekelezwa tena kwa nguvu zote ili kuona tunadhibiti hali hiyo”alisema.
Naye afisa mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba Ibrahim Saleh Juma, alisema kwa upande wa viwanja vya ndege, tayari wameshaweka mikakati ya kuhakikisha abiria waote wanaosafiri wanapaswa kuvaa barakoa, pamoja na kunawa mikono wanapokua katika eneo la viwanja vya ndege.
Alisema jambo jengine ni kuhakikisha wanaongeza madaktari na vifaa vya kupimia joto, ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi zaidi pamoja na abiria kufuata miongozo yote ya wizara ya afya.
Akizungumzia eneo la bandarini, Mdhamini Ibrahim alisema wanakusudia kukutana na watendaji wa makampuni ya meli zinazotoa huduma katika bandari ya mkoani na wete, ili kuweza kuepusha msongamano wa abiria wakati wa meli mbili zinapokuwepo bandari kwa ajili ya kupakia abiria.
“Sisi tumeomba katika eneo hili kuongezewa mashine za kupimia pamoja na madaktari, huku tukiendelea kuvitum ia vituo vyetu vya afya vilivyopo bandarini katika utoaji wa huduma”alisema.
Hata hivyo aliwataka abiria wote wanaotumia usafiri wa baharini au angani, kuhakikisha wanafuata taratibu zote na miongozo iliyoweka ili kudhibiti wimbvo la tatu la Covidi 19.
Kwa upande wake afisa ya afya Jinsia ustawi wa jamii wazee na watoto Pemba Yakub Mohamed Shoka, alisema tayari utaratibu wameshauweka katika ameneo yote yenye mikusanyiko ya watu, kwa kuweka mashine maalumu za kujifukizia na kupimia Covod 19.
“Tumejipanga kutoa elimu kwa wananchi katika ameneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba, tunatarajia kuwa na mkutano mkubwa wa watendaji wote Jumatatu”alisema.
Aliwataka wananchi kuendelea kujikinga kwa kuhakikisha wanavaa barakoa wakati wote wanapokuwa katika vyombo vya usafiri, pamoja na mikusanyiko ya watu sambamba na taasisi za serikali kuweka vitakasa mikono na ndoo za maji yenye kutiririka.