· Ni baada ya kuzindua mfumo mpya wa malipo kwa wakulima wa karafuu kupitia huduma ya Ezypesa. |
|
|
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NA ABDI SULEIMAN.
WAZIRI wa biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, amesisitiza kuwa Serikali imeingia rasmi katika matumizi ya mifumo ya kidigitali ya malipo huku akiwataka wananchi kuwa tayari kuendana na mabadiliko hayo.
Aliyasema hayo wakati akizindua mfumo mpya wa malipo kwa wakulima wa karafuu kupitia huduma ya Ezypesa ambapo wakulima watalipwa malipo yao kwa njia ya simu tofauti na ilivyo sasa.
Alisema serikali imeamua kutumia mifumo ya kidigitali katika malipo na makusanyo yate ya fedha, kama ilivyo tolewa na Waziri wa Fedha barazani mwaka huu.
Waziri Omar alisema hakuna fedha yoyote ya mkulima itakayotolewa mkononi, bali wakulima watalipwa fedha zao kutumia Mfumo wa Ezypesa huku akiyataka mashirika hayo kujidhatiti katika mifumo yao ya malipo isije ikawa ni changamoto kwa wakulima wakati wakuhitaji fedha zao.
Hayo aliyaelea huko bandarini wete, kwenye hafla ya uzinduzi wa msimu wamanunuzi ya Karafuu kwa mwaka 2021/2022, ukiambatana na uzinduzi wa uchumaji wa zao hilo.
“Suala la mfumo wa malipo hapa lazima wananchi na wakulima mufahamu, serikali imeamua kwenda na mfumo wakidigitali kuanzia mwaka huu, hakuna fedha itakayotoka mkononi fedha zitatumia mifumo ya kisasa”alisema.
“Tunajua mfumo huo ndio umeanza na mgeni kwetu sisi, unaweza kuleta changamoto, changamoto zitakazojitokeza zitatatuliwa kwa wakati”alisema.
Aliwataka zantel na PBZ kujipanga kikamilifu kuhakikisha mifumo ya malipo inakuwa sawa na wananchi hawapati matatizo wakati wanakupokea malipo yao.
kwa upande wake Afisa Mkuu wa Fedha Zantel Azizi Said Ali, alisema kampuni ya Zantel iko msstari wambele katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora za kidigitali na bei nafuu, ili kurahisisha maisha kwenye ulimwengu wa sasa wa kidigitali.
“Nidhahiri kuwa dunia inakwenda kwa kasi sana katika matiumizi ya teknolojia za kidigitali, kama kufanya malipo, manunuzi ya bidhaa na huduma, zantel kupitia Ezypesa tumeliona hilo na tumeendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wananchi”alisema.
Hata hivyo alilishukuru shirika la biashara la taifa ZSTC, kwa kuingia makubaliano ya ushirikiano kwa lengo la kurahisisha malipo kwa wakulima wa zao la karafuu Kisiwani Pemba.
Hata hivyo aliwataka wakulima wa karafuu kuhakikisha wanajiunga na huduma za Ezypesa ili kupata huduma hiyo itakayo warahisishia mambo mengi ikiwemo muda wa kwenda kutoa fedha umbali mrefu, kwani mawakala wa Ezypesa wapo katika maeneo yote ya kisiwa hicho.
“Baada ya fedha za mauzo kupokelewa katika akaunti za ZSTC, Zantel kupitia Ezypesa itahamisha malipo hayo moja kwa moja kwa wakulima ambao wamejisajili, wakulima watapata taarifa za malipo hayo kupitia ujume wa SMS”alisema
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazinii Pemba Salama Mbarouk Khatib, alisema ZSTC ndio shirika pekee lililopewa mamlaka ya kununua karafuu na sio taasisi nyengien.
Naye mkuu wa Mkoa wa Kaskazinii Pemba Salama Mbarouk Khatib, alisema ZSTC ndio shirika pekee lililopewa mamlaka ya kununua karafuu na sio taasisi nyengien.
Aidha alilitaka shirika hilo kununua karafuu kwa wakulima na sio sehemu nyengine, sambamba na kuondokana na udanganyifu na kuwa makini katika suala la upimaji ili kuondosha matatizo yanayojitokeza.
katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Dkt.Islam Seif Saleh, alisema serikali ya awamu ya nane iliahidi neema kwa wakulima na imeanza kutekeleza, kutokana na kuwa inawajali wananchi wake.
Aidha alisema Serikali iko imejipanga vizuri na itahakikisha utaratibu unafuatwa, “Serikali iko macho na imejipanga kikamilifu kuhakikisha inadhibiti magendo yote ya karafuu, nawasihi wakulima na wafanya biashara kuwa wazalendo, kwa nchi yao ili iweze kunufaika na matunda ya karafuu”alisema.
Akizungumzia suala la malipo, alisema Serikali iliona fedha nyingi zinatumika katika uchumaji wa karafuu, ndio maana imeamua kuja na mfumo wa malipo kidigitali kwa kutumia Ezypesa au benk na sio fedha mkononi.