Monday, November 25

Jeff Bezos: Ijue siri ya mafanikio ya mtu tajiri zaidi duniani

Mwaka 2004, Jeff Bezos na mshauri wake wa masuala ya kiufundi Colin Bryar walisafiri pamoja hadi mji wa Tacoma, umbali wa saa moja kusini mwa jiji la Seattle jimbo la Washington.

Wakati huo, thamani ya kampuni ya Amazon ilikuwa mabilioni ya dola. Hata hivyo, walikuwa wanaelekea katika kituo cha kuhudumia wateja cha kampuni hiyo – kwa siku mbili walifanya kazi kama watoa huduma kwa wateja.

“Jeff alikuwa akipokea simu zinazopigwa na wateja yeye mwenyewe,” Bryar anasema. Anakumbuka malalmiko ya moja ya bidhaa yalivyokuwa yakiendelea kuripotiwa kila wakati. “Jeff alishituka. Macho yalimtoka.”

Bezos alikuwa ametatizika. Bila shaka yoyote bidhaa hiyo ilikuwa na hitilafu, lakini suala hilo halikuripotiwa katika ngazi za juu.

Baadaye siku hiyo hiyo, alituma ujumbe kwa njia ya barua pepe akitaka apewe mapendekezo ya namna gani ya kuripoti bidhaa zenye matatizo sokoni.

Bezos anajiuzulu wadhifa wake kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Amazon leo Jumatatu – ikiwa ni miaka 27 kamili toka alipoianzisha kampuni hiyo.

Kwa wakati wote huo wa takribani miongo mitatu alikuwa ameanzisha kanuni kadhaa za uongozi zisizo za kawaida – ambazo baadhi wanasema kwamba ndizo zilizokuwa msingi wa mafanikio yake.

A product sits on a conveyer belt in an Amazon warehouse

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wengine wanaamini kuwa walizungumzia kila hatua ambayo haikuwa sawa katika kampuni hiyo kubwa.

Zungumza na yeyote yule ambaye aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya Amazon, na hutachukua muda mrefu kabla ya kusikia neno “kupenda wateja kupita kiasi”.

Kwa Bezos, faida ilikuwa ni azma ya kipindi cha muda mrefu. Kwa kampuni kufanikiwa lazima wateja wake wafurahi – yaani kwa vyovyote vile.

Nadia Shouraboura alianza kufanya kazi Amazon mwaka 2004. Na ilifika wakati akaalikwa katika kikao cha mameneja wa Amazon – ambayo ndiyo bodi kuu ya usimamizi. Lakini alipoanza kuzungumza, alifikiria kwamba haitachukua muda mrefu kabla ya kufutwa kazi.

“Nilifanya makosa makubwa sana wakati wa kilele cha msimu wa Krismasi,” anasema.

Shouraboura alikuwa ameagiza bidhaa za msingi kwenya rafu za ghala ambazo zilikuwa juu kabisa. Ingegharimu pesa na muda mwingi kupata bidhaa sahihi kwenye rafu hizo.

“Nikajiwa na wazo la kijanja la kutumia pesa kidogo ili kutatua tatizo hilo. Lakini baada ya kumuelezea Jeff, aliniangalia na kusema, ‘fikra zako kuhusu hili sio sawa kabisa’.”

“Wewe unafikiria namna ya kubana matumizi hapa. Tatua tatizo la wateja, kisha urejee kwangu ndani ya wiki chache na unipe gharama zote.”

Madai ya kushutusha

Bezos ana wakosoaji wengi. Mwezi uliopita, makala iliyoshangaza wengi ilichapishwa na gazeti la ProPublica ilidai kuona malipo ya kodi ya mapato ya Bezos na kudai kuwa tajiri huyo hakulipa kodi kabisa mwaka 2007 na 2011. Lilikuwa dai la kustaajabisha sana dhidi ya mtu tajiri zaidi duniani.

Simulizi zingine hasi kuhusu Amazon, ni juu ya madai ya unyama ndani ya kampuni hiyo, pia kuna madai ya kuhodhi soko, ambayo yote kwa pamoja yameathiri sifa ya Bezos.

Hata hivyo, watu wengi ambao walifanya kazi kwa karibu naye hawakubaliani na madai ya kuwa Bezos hajali watu au ni mbinafsi.

Kwao wao ni mtu mwenye maono ya biashara – mtu mwenye lengo kuu ambaye filosofia yake ni ya kupigiwa mfano na kujenga kampuni yenye thamani ya karibu dola trilioni 1.8.

Kanuni ya kulisha watu wote kwa pizza mbili tu

Bezos napenda kufanya kazi na timu ndogo. Amekuwa akihakikisha katika utawala wake, mikutano inakuwa na tija: hakikisha unaweza kulisha timu yote kwa pizza mbili tu.

Anachukia mawasilisho au mapendekezo kwa njia ya uwasilishaji ukutani ama ubaoni kwa njia ya ‘PowerPoint’ na badala yake anapendelea taarifa zilizoandikwa kwa ajili ya watendaji kujadili.

Ili kuepusha watu wachache kuwa wao ndio wanaongea tu mkutanoni, wakati fulani alichukua muda wake kumuuliza kila mmoja mawazo yake kuhusu suala fulani.

Bezos

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Na watu wanasema kuwa yeye hupendelea wale wanaokosoa, kupinga au kuja a mawazo tofauti. “Tungejadiliana na kubishana lakini mwisho kuja na mawazo tofauti baina yetu,” anasema Shouraboura.

“Kila kitu kinakuwa wazi wakati wa majadiliano, na majadiliano yanapamba moto na kuibua shauku za watu. Lakini ni kuhusu suala linalojadiliwa wala sio dhidi ya mtu fulani” anasema.

Kampuni ya Amazon ina “kanuni 14 za uongozi” ilizojiwekea. Moja wapo ni “msingi wa wazungumzaji kutofautiana katika suala fulani”.

Na yumkini kuwa Bezos, hakika kabisa anataka kuendeleza utamaduni huo hata katika ngazi ya juu zaidi. Viongozi wanastahili “kutofikia makubaliano tu kwa sababu ya mshikamano wa kijamii”, kanuni hiyo inasema.

Hata hivyo, hayo ndio maswali kuhusu ikiwa filisofia hiyo huwa inafasiriwa vizuri na wafanyakazi wa ngazi ya chini wa kampuni hiyo.

Mwaka 2015, gazeti la New York Times lilichapisha makala iliyokuwa na madai ya uwepo wa “utamaduni wa mkwaruzano kazini” kutoka kwa waliokuwa wafanya kazi.

Bezos mwenyewe anapendelea sanan masuala ya uhandisi, uvumbuzi na mashine.

Anaguswa sana na mambo ya mahesabu – kufuatilia mambo kwa kuzingatia gharama zake na faida zake halisi, sio sifa mbaya katika ulimwengu wa biashara yenye kuhusisha usafirishaji. Lakini wakosoaji wake wanasema kwamba upendeleo huwa una gharama zake kibinadamu, hasa kwa kuzingatia maghala kadhaa ya Amazon.

Andy Jassy

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,Andy Jassy amefanya kazi na Amazon toka mwaka 1997 na sasa namrithi Bezos kuingoza Amazon

Baada ya kushindwa kwa jaribio la wafanyazi wa kampuni hiyo huko Bessemer, Alabama, kuunda muungano, nilizungumza na wafanyakazi wengi waliodai kile kilichoonekana kuwa “sehemu ndogo tu kati ya kampuni kubwa”. Wengine walielezea hisia ya “kufuatiliwa kila wakati.”

Katika ngazi ya uongozi wa juu, mtindo wa usimamizi wa Bezos ulionekana kuwa tofauti. Anapenda timu yake kuwa na uhuru, ambao anaamini kwamba ndio msingi mzuri wa ubunifu.

Kampuni ya utoaji huduma za kimtandao ya Amazon kama vile uhifadhi wa data ambayo imekuwa na mafanikio makubwa, haikuwa na uhusiano wa karibu sana na kampuni kuu ile ya biashara ya mtandaoni.

Hata hivyo, Bezos aliunga mkono wazo hilo na kumpa uhuru mfanyakazi aliyemuamini Andy Jassy pamoja na mtaji, ili kuanza kuunda kampuni ndani ya kampuni.

Bezos anamchukulia Jassy kama mjasiriamali, sio tu kwamba ni meneja – na hiyo ikiwa sababu kuu kwanini atachukua nafasi yake kama Afisa Mtendaji mkuu wa Amazon.

“Ni rahisi sana kuwa jasiri wakati unaanza biashara yako” amesema Shouraboura. “Wakati unaendelea kuikuza, inaendelea kuwa vigumu zaidi kuendeleza ujasiri kwa sababu sasa kuna mengi yanayokuwa katika hatari. Kila wakati alikuwa jasiri.”

Watu wanaomjua wanasema kuwa Bezos alipendelea sana kutatua matatizo kwa kwenda “kinyume nyume. Ni mchakato maalum sana katika kampuni ya Amazon,” Bryar amesema.

Katika hatua ya mipango, timu zitatengeneza matukio kwenda kinyume – na kuanza na vile mwanzo utakavyokuwa na kisha kwenda kinyume.

Jeff Bezos addresses the media next to the New Shepard launch vehicle

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,Jeff Bezos na kaka yake Mark wataenda naga za mbali kwa chombo kilichotengenezwa na kampuni yake Julai 20.

“Cha kwanza kabisa timu hufanya ni kuandika taarifa kwa vyombo vya habari, ambacho kawaida huwa cha mwisho kufanyika na kampuni zingine.”

Hatua hii iliendana na mtazamo wa muda wa Bezos. Ni jambo analolifikiria sana. Aliwekeza dola milioni 42, kujenga saa ya miaka 10,000 kwenye mlima mmoja huko Texas. Ilitakiwa kuwakilisha nguvu ya “ufikiriaji wa muda mrefu.”

Bezos hufurahishwa sana na safari za anga la mbali na baadaye mwezi huu analenga kusafiri kwenda anga la mbali kwa kutumia ndege ya kwanza yenye abiria iliyotengenezwa na kampuni yake ya Blue Origin.

Pingamizi la hiari la kumzuia kurejea tena dunia limesainiwa na karibu watu 150,000.

Mpende ama mchukie, Bezos amethibitisha kuwa kiongozi mtendaji na mwerevu hasa – mtu ambaye amebadilisha jinsi kampuni zinavyofanya kazi ulimwenguni.