Sunday, November 24

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 06.07.2021: Ramos, Varane, Camavinga, Coman, Messi, Ronaldo, Griezmann

Sergio Ramos

Mlinzi wa kihispania Sergio Ramos, 35, atafanyiwa vipimo vya afya jijini Paris Jumanne hii kabla ya kujiunga na Paris St-Germain kama mchezaji huru kufuatia kuondoka kwake Real Madrid. (ESPN)

Mtendaji wa Bayern Munich Oliver Kahn ana uhakika wa kumbakiza klabuni hapo winga mfaransa Kingsley Coman licha ya Liverpool kuonyesha nia ya kumtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (Mirror)

Manchester United wanajiandaa kutoa dau la £50m kwa ajili ya mlinzi wa Real Madrid, Mfaransa Raphael Varane, 28, na £25m kwa ajili ya kiungo wa Ufaransa anayekipigia Rennes Eduardo Camavinga, 18, wakati huu wakiendelea kumwaga pesa kujenga kikosi chao. (Marca via Mail)

Raphel Varane

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Mario Balotelli, 30, anajiandaa kujiunga na klabu ya Adana Demirspor ya Uturuki, akiwa na imani ya kurejea kwenye timu ya taifa kwa ajili ya fainali za mwakani za kombe la dunia. (Goal)

Paris St-Germain imempa ofa ya kumpeleka Ufaransa Muargentina Lionel Messi baada ya mkataba wake na Barcelona kukoma wiki iliyopita. Gwiji huyo wa Nou Camp mwenye miaka 33 ameisaidia nchi yake kufuzu nusu fainali ya Copa America licha ya sintofahamu ya mustakabali wake. (Mail)

Messi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Lionel Messi

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Mfaransa Antoine Griezmann, 30, anaonekana kuwa chaguo linalowezekana kwa Manchester City msimu huu iwapo City watashindwa kumnasa mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na England Harry Kane, 27. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Juventus wanataka kumrejesha kiungo wake za zamani anayechezea Manchester United, Paul Pogba, 28, msimu huu. Wakali hao wa Italia wanataka kumrejesha Turin mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa miaka mitano tangu aondoke kwa uhamisho ulioweka rekodi ya dunia. (90Min)

Paul Pogba
Maelezo ya picha,Paul Pogba

AC Milan wanajiandaa kuanza mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho mwingine wa mkopo wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Tiemoue Bakayoko, 26. (Corriere dello Sport – in Italian)

Liverpool inaongoza harakati za majaribio ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa na PSG, Kylian Mbappe. Tetesi zinaendelea kuhusu mustakabali wa kinda hilo lenye miaka 22, ambaye amebakiza mwaka mmoja tu wa mkataba wake pale Parc des Princes. (ESPN)

Mbappe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Kylian Mbappe

Meneja mpya wa Crystal Palace, Patrick Vieira ana matumaini kwamba kiungo wa Scotland na Celtic Ryan Christie atakuwa usajili wake wa kwanza pale Selhurst Park. Nyota huyo mwenye miaka 26 anawaniwa pia na klabu ya zamani ya Vieira, Nice. (Daily Record)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika wa kumbakiza Emile Smith Rowe pale Emirates licha ya ushawishi mkubwa kutoka Aston Villa. Villa inajiandaa kuongeza dau kwa ajili ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 20, baada ya dau la mwanzo la £30m kukataliwa. (Mirror)

Emile Smith Rowe
Maelezo ya picha,Emile Smith Rowe

Kocha mpya wa Tottenham Hotspur,Nuno Espirito Santo anataka kumnasa mshambuliaji wa Switzerland,Haris Seferovic. Benfica inataka kumpiga bei mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Mirror)

Inter Milan wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa kushoto wa Kigiriki, Kostas Tsimikas kutoka Liverpool. Tsimikas, 25, alijiunga na Liverpool msimu uliopita, na mpaka sasa amefanikiwa kuichezea klabu hiyo michezo saba tu katika mashindano yote. (Calciomercato, in Italian)