Wednesday, January 15

FAMILIA ya Amed Alfalas, kutoka Dubai na wasaidizi wake wamewasili Kisiwani Pemba.

Na Shaib Kifaya  Pemba.

FAMILIA ya Amed Alfalas, kutoka Dubai akiongoza na wasaidizi wake  Umewasili Kisiwani Pemba na kutembelea hospital  tofauti  kwa lengo la kuangalia Changamoto  na kuzisaidia.

Hayo yamelezwa na Waziri wa afya Ustawi Wajamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar, Nasoor Ahmed Mazrou,  wakati wa Ziara hiyo huko hospital ya Vitongoji Cottage.

Alisema lengo la Mfadhili huyo Armed Alfalas Kutoka Dubai ni  kusaidia Vifaa tiba na mashine mbali mbali  kwa hospital  kwa vile ameona kuna mapungufu makubwa yanayohitajika wakati wa utoaji wa huduma kwa wananchi na kuahidi kujenga kituo cha Usafishaji damu cha Wagonjwa wenye matatizo ya Figo ili kuepuka gharama za kwenda Unguja kimatibabu pamoja na kuahidi kujenga jengo la mama na mtoto na kutoa mashine mbali mbali  za uchunguzi kwa hospital za Pemba

”  Kwa kweli kuja Ujumbe huu wa familia ya bwana Armed Alfalas imetupa matumaini makubwa kwetu Kwan ametuahid mambo mengi yenye mafanikio kwa maslahi ya wananchi wetu na serikali yetu “alisema Waziri Mazour

Nae  Ahmed Alfalas  kutoka Dubai, alisema lengo  la Ziara kwa Visiwa  viwili vya Unguja na Pemba, ni kutembelea hospital na kuangalia changamoto zilizomo na kuweza kusaidia.

Akizungumzia kwa Upande wa Pemba kwenye ziara hiyo alibaini kunamapungufu makubwa sana kwa hospital na kusema anategemea kujenga kituoa Kikubwa cha Uchunguzi wa damu kwa wagonjwa wanao sumbuliwa na maradhi ya figo ili kupunguza gharama za kwenda matibabu Unguja kutokana na hali zao kuwa duni  pamoja na kuahid kujenga jengo la mama na mtoto hospital ya Cottage Vitongoji kutokana na uhaba wa nafasi kwa mama wajawazito.

Kwa Upande wake Afisa Mdhamini wa Wizara ya Afya  Ustawi WA Jamii, Wazee  Jinsia na Watoto  Yakoub Muhammed Shoka  ,alisema kwa Upande wa serikali utahakikisha wanatoa mashirikiano na Ujumbe huo muda wote kwa yale ambayo ameahidi kuwasaidia.

Akitoa neno la shukurani kwa Ujumbe huo daktar dhamana wa hospital ya Cottage ya Vitongoji Sharif Hamad Khatibu  alisema  ziara ya Ahmed Alfalas, Kutok Dubai imewapa matumaini makubwa kwani ameahidi kuwapatia mashine na vya Uchunguzi na vifaa tiba ambavyo kwao ni muhimu sana kwa shughuli za utoaji wa huduma kwa jamii

Katika ziara yake hiyo Waziri na Ujumbe huo walitembelea hospital ya Cottage Vitongoji na Micheweni, Wete hospital .