Chelsea wanajiandaa kutoa kitita cha £150m kwa ajili ya mshambuliaji wa Borussia Erling Braut Haaland na tayari klabu hiyo ya Stamford imeshafanya mazungumzo na upande wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway. (90 Min)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo “haiwezi kumudu gharama” za mshambuliaji mpya na “kuna kila dalili” mabingwa hao wa ligi kuu England wasisajili mshambuliaji msimu huu. (TVS, via Mail)
Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti ameiambia klabu hiyo angetamani kumsajili mshambuliaji wa Kibrazil Richarlison, 24, kutoka klabu yale ya zamani ya Everton. Klabu hiyo ya La Liga inaangalia kama hilo linawezekana. (ESPN)
Wakala wa kiungo wa Chelsea Jorginho, 29, anasema zipo timu zinazomuhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia lakini anatarajiwa kuongeza mkataba mpya wa kusalia ‘the Blues’ zaidi ya mwaka 2023. (Radio Marte, via Metro)
Nahodha wa RB Leipzig Marcel Sabitzer, 27, anaweza kupatikana kwa ada ya £17m, wakati huu kiungo huyo wa Austria akiingia miezi yake 12 ya mwisho ya mkataba wake na mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakiwa bado yanasuasua. (90 Min)
Wolves imekubali kumuuza beki wake wa kireno, Ruben Vinagre, 22, kwenda Sporting Lisbon kwa ada ya £8.6m. (Football Insider)
Tottenham wanamfuatilia beki wa Sassuolo Mert Muldur, huku West Ham wakitajwa kumtaka pia nyota huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 22. (Mail)
Klabu ya Paris St-Germain imejikuta kwa bahati mbaya ikithibitisha kumsajili beki wa kati wa Hispania Sergio Ramos, 35 ambaye ameondoka Real Madrid baada ya mkataba wake kumalizika, kwa kuchapisha usajili wake kwenye mtandao wa klabu hiyo kabla ya muda uliopangwa wa Alhamis. (Goal)
Southampton wana uhakika wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Kiingereza Adam Armstrong, 24, kutoka Blackburn Rovers kwa ada ya £10m. (Football League World)
Middlesbrough iko katika mazungumzo mazuri ya kumsajili kiungo wa Atletico Banfield Martin Payero, ambaye yumo kwenye kikosi cha Argentina kitakachoshiri michezo ya Olympic huko Tokyo msimu huu. (Football Insider)
Meneja wa Bayern Munich Julian Nagelsmann amesema kiungo wa Ujerumani Leon Goretzka, anayehusishwa kutakiwa Manchester United, ni mchezaji “muhimu” wa klabu hiyo na “atafurahi kufanya naye kazi kwa miaka mingi ijayo”. (Goal)
AC Milan itaongeza dau lake kwa ajili ya kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie wakijaribu kuongeza mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport)
Kiungo wa Italia Davide Calabria, 24, amekubali kusaini mkataba mpya, utakaombakiza AC Milan mpaka 2025. (Calciomercato, via Football Italia)