NA ABDI SULEIMAN.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuwa kwamujibu wa sheria iliyoanzisha shirika la miashara la Taifa (ZSTC), kua ndio shirika pekee lenye mamlaka ya kununua karafuu pekee ya kununua karafuu za Zanzibar moja kwa moja kutoka kwa wakulima.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, hivi karibuni katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa manunuzi ya karafuu mwaka 2021/2022, iliyofanyika bandarini Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aidha waziri huyo wa Biashara alisema wananchi wanapaswa kufahamua kuwa hakuna taasisi au chombo chengine kilichopewa mamlaka ya kununua karafuu za Zanzibar moja kwa moja kutoka kwa wakuliza zaidi ya shirika la ZSTC.
Waziri Omar alipiga maruku kwa wananchi wananchi kuuza karafuu kwa mtu mwengine yoyote, hivyo wanapaswa kutambua kuwa ZSTC haina madalali wala mawakala iliowatuma kununua karafuu hizo.
“Serikali imeweka utaratibu mzuri karafuu kuziuza kwa wakati tena salama, ZSTC ndio sehemu pekee ya kuuzia karafuu hizo tena wanazifuata popote zilipo”alisema.
Akizungumzia suala la dhamana kwa wanaopasisha na kuweka ubora, aliwataka kutambua wamepewa dhamana kubwa hiyo, kuhakikisha wanatekeleza dhamana zao bila ya kumuonea mkulima wala kujionea wao katika upasishaji na upandishaji wa gredi.
Alisema bado karafuu ya Zanzibar inaendelea kuwa muhimu katika soko la dunia, hivyo aliwataka wakulima kuhakikisha wanazikichuma zikiwa zimepea, pamoja na kuzianika katika mazingira mazuri ili kuendelea kulinda ubora wake.
Alifahamisha kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kuzichuma karafuu zikiwa change, pamoja na kuzianiaka sehemu zilizokuwa sio salama hivyo wanapaswa kutambua kuwa karafuu pia ni chakula kwa baadhi ya nchi.
“Kumejitokeza tabia ya watu kuzichuma karafuu change, hilo lisifanywe maana halimsaidi mmiliki, nchi bali tunapaswa kuwa na uzalendo kwa nchi, kama karafuu hazijawa tayari tunapaswa kuziwacha mpaka zipee, ili tusipoteze hadhi ya karafuu yetu kila nchi inajivunia vitu vyake”alisema.
“Ikiwa tutazianika barabarani, kuzichuma change tutaziporomosha bei na kuzitia ila na sifa mbaya, mwisho wake tutakosa soko katika soko la dunia, mapato tutayakosa serikali itashindwa kufanya shuhuli zake”alieleza.
Hata hivyo Waziri huyo, alisema serikali imeendelea kulipa hadhi zao hilo, kwani ndio linaloipatia fedha zakigeni ikifuatiwa na utalii, pamoja na karafuu kutengeneza ajira nyiki kwa vijana muda uwa uchumaji unapofika.
“Kila nchi zinategemea rasilimali zake kama vile gesi, almasi, zahabu, mafuta, sisi Zanzibar tunategemea karafuu zetu, hivyo tunapaswa kudhithamini ili ziendelee kutufaa”alisema.
Alisema wako katika makakati wakuhakikisha kilimo cha karafuu kina kua na tija na kuongeza uzalishaji, kwani wanaamini karafuu bado ni dhahabu, almasi yetu lazima tuilinde.
Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, aliwataka wananchi kutambua kuwa serikali imejipanga na iko macho, wasitegemee kupata nafasi ya kusafirisha magendo ya karafuu.
Alisema katika kulia mkazo suala hilo, tayari mikakati mbali mbali imeshapangwa ili kuhakikisha magendo hayatokuwepo, huku akiwataka wananchi wanaojihusisha na suala la magendo kujisalimisha mapema pamoja na kuachana na biashara hiyo.
Mkurugenzi wa ZSTC Said Seif Mzee, alisema serikali imechukua juhudi kubwa sana licha ya kushuka kwa bei ya zao hilo, katika soko la dunia lakini serikali imeendelea kusimamia bei yake ya gredi ya kwanza shilingi elfu 14000/= kwa kilo, gredi ya pili kilo shilingi elfu 13000/= na gredi ya tatu kilo shilingi elfu 12000/=.