NA KHADIJA KOMBO -PEMBA
Wanawake nchini wametakiwa kufahamu kwamba wana haki ya kugombania nafasi za uongozi katika Nyanja zote hivyo wasijikite kugombea katika nafasi za kisiasa pekee.
Akizungumza katika kikao cha tathmini juu ya mafanikio na changamoto katika kazi za uhamasishaji wa wanawake kugombea nafasi za uongozi huko katika Ofisi za Jumuiya ya waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA kwa upande wa Zanzibar Ofisi za Pemba, Afisa Ufatiliaji jumuiya hio Mohammed Khatib Mohammed amesema wanaweke wengi hujikita kugombea nafasi za kisiasa tu lakini hawazingatii uwezekano wa kukamata nafasi nyengine ndani ya taasisi.
Kwa upande wake Mratibwa TAMWA Pemba Fat-hiya Mussa Said amesema uzoefu umeonesha kwamba wanawake wengi waliojitokeza katika kugombea nafasi hizo ni wale ambao wanatokea katika asasi za kiraia hivyo kuna kazi kubwa kwa wanaharakati kuwa hamasisha wanawake kujiunga na asasi mbali mbali za kiraia.
Wakizungumzia kuhusu matatizo yaliyojitokeza katika uhamasishaji wa kipindi kilichopita wanaharakati hao wamesema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kutoyafikia maeneo ya mbali , na rushwa ambayo bado inaendelea kuwaathiri wanawake.
Kuangalia videi hii bofya hapo chini