Tuesday, November 26

KAMATI ya Mendeleo ya jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, imepitisha utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya jimbo la hilo.

MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake Bakari Hamad Bakari, akikagua banda la skuli ya maandalizi Ditia Jimbo la Wawi, kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo makubwa hadi kukamilika kwake, baada ya kupitishwa na kamati ya jimbo.
BAADHI ya wajumbe wa kamati ya jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake wakikagua, skuli ya maandalizi Kibokoni Vitongoji skuli hiyo tayari imeshapangwa na kamati hiyo kumalizwa ujenzi wake, kupitia mwakilishi na mbunge wa jimbo hilo
MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Wilaya ya Cjke Chake Bakari Hamad Bakari, akizungumza na wananchi wa Kibokoni Vitongoji mara baada ya kukagua ujenzi wa skuli ya maandalizi Kobokoni, ambayo inahitaji kuezekwa kwa sasa kupitia mwakilishi na Mbunge wa jimbo hilo.(
WANANCHI wa shehia ya kibokoni Vitongoji wakimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, wakati alipofika kukagua ujenzi wa banda la skuli ya maandalizi kibokoni, ambayo imo katika mkakati wa kumaliziwa ujenzi wake na mwakilishi wa jimbo hilo.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

NA ABDI SULEIMAN.

KAMATI ya Mendeleo ya jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, imepitisha utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya jimbo la hilo, ili kutekelezwa ndani ya kipindi cha miezi miwili hii.

Miradi iliyopitishwa na kukaguliwa na wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na ukarabati wa banda la vyumba viwili na ofisi za skuli ya maandalizi ditia, banda la vyumba viwili na ofisi skuli ya maandalizi Kibokoni Vitongoji, uwekaji wa kifusi katika barabara ya Mvumoni hadi fura KM 1.5 na ukarati wa uwanja wa mpira gombani ya kale.

Akizungumza mwananchi katika maeneo hayo, Mwalikishi wa jimbo la Wawi Bakari Hamad Bakari alisema utekelezaji wa miradi hiyo ni kutokana na ahadi zao walizoziweka kwa wananchi wa maeneo hayo wakati walipokua wakiomba kura, kwamba wataimaliza au kuitekeleza ikiwa sasa ndio kipindi chake.

Alisema ndani ya kipindi hiki cha miezi miwili, viongozi wa jimbo hilo mwakilishi na mbunge wamejipanga kuhakikisha miradi hiyo inamalizika kwa wakati muwafaka.

“Sisi tuliahidi na sasa tupo tayari kutekeleza yale yote tulioahidi, wananchi tunapaswa kufahamu kuwa jimbo letu ni kubwa na linachangamoto nyingi ila tutazitatua kidogo kidogo”alisema.

Alisema kukamilika kwa mabanda hayo yataweza kuwapunguzi wanafunzi masafa marefu kwenda kusoma maeneo ya mbali, jambo ambalo litaweza kuwasaidia wavijana hao.

“Inapokuja miti na bati kwa ajili ya kuezeka, nawaombeni wananchi tujitokeze kwenda kqwenda kuibeba wenyewe kwani itakuwa gari haifiki mapaka ilipo skuli, kutokana na miundombinu kuwa haiku rafiki”alisema.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Wawi Khamis Kassaim, aliwataka wananchi wa mvumoni na furaha kuwa kitu kimoja wakati wa ukarabati wa barabara yao utakapofika.

Alisema kwa wananchi wanaswa kuwa kitu kimoja kwa sasa katika suala la maendeleo, kwani maendeleo yanapokuja hayachaguwi siasa wala chama.

Khamis Juma na Yahya Said walisema kipindi cha mvua ni vigumu barabara hiyo kupitika, hivyo viongozi wanapaswa kuangalia kwa jicho la huruma ukarabati wa barabara hiyo.

“Sisi itakavyofanywa vyovyote pia ni sawa sisi tunachohitaji ni kupitika kwa barabara yetu, ila vizuri kuwekewa vifusi katika mashimo yote na sisi tupo tayari kushirikiana na uongozi huo”alisema.

Nao wananchi wa Kibokoni Vitongoji wamewataka viongozi hao kuwaangalia na suala la barabara ya kijijini kwao, kwani inaponyesha mvua inakuwa ni usumbufu kwa watoto kwenda skuli.