Manchester City wataachana na mipango ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 27, endapo watafanikiwa kumnasa winga machachari wa Aston Villa, Jack Grealish, 25. (Manchester Evening News)
Kiungo raia wa Colombia James Rodriguez, 30, ameelezwa kuwa hayupo kwenye mipango ya kocha mpya wa Everton Rafael Benitez, na kwamba yupo huru kuhama klabuni hapo endapo ofa nzuri itawasilishwa. (Liverpool Echo)
Klabu ya Atletico Madrid imepiga hatua mojja mbele ya Arsenal katika mbio za kumsajili mshambuliajji machachari wa Inter Milan na timu ya taifa ya Argentina Lautaro Martinez ambaye ana thamani ya Euro milioni 90. (Tuttosport – in Italian)
Ofa ya pauni milioni 43 iliyotolewa na klabu ya Tottenham kutaka kumsajili beki wa Agentina Cristian Romero imekubaliwa na klabu ya Atalanta. (Talksport)
Leeds wamo katika mipango ya kutaka kumsajili winga raia wa Uhispania anayechezea klabu ya Wolves, Adama Traore, 25, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30. (Goal)
Klabu ya Tottenham ambayo sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Wolves, Nuno Espirito Santo pia inapiga hesabu za kutaka kumsajili Traore. (Mail)
Klabu ya West Ham ingali katika mazungumzo na klabu ya Chelsea juu ya usajili wa beki wa kati raia wa Ufaransa Kurt Zouma, 26, japo West Ham inahangaika kufikia dau linalotakiwa na Chelsea. (Sun)
Endapo West Ham itashindwa kumsajili Zouma kutoka Chelsea, basi mbadala wake wanapanga awe beki raia wa Serbia Nikola Milenkovic anayechezea klabu ya Fiorentina.
Klabu ya Crystal Palace inataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji kutoka England Ademola Lookman, 23, anayechezea katika klabu ya RB Leipzig. Mipango ya Palace hata hivyo huenda ikakumbana na upinzani kutoka vilabu vya Burnley na Watford. (Sun)
Ajenti wa beki wa Tottenham Davinson Sanchez, 25, amefanya mazungumzo na klabu ya Sevilla ili beki huyo kuhamia katika klabu hiyo. Sanchez raia wa Colombia amekuwa akinyemelewa na Sevilla ili kuchukua nafasi ya Jules Kounde, 22 ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Chelsea. (Caracol Radio via Mail)
Klabu ya Wolves imeweka wazi nia yake ya kutaka kumsajili kiungo wa Wales Aaron Ramsey kutoka miamba ya Italia Juventus, hata hivyo kiungo huyo wa zamani wa Arsenal mwenye miaka 30 anaripotiwa kutoshawishika na ofa hiyo. (Calciomercato – Italian)
CHANZO CHA HABARI BBC