Wednesday, January 15

Fahamu majengo 10 marefu zaidi barani Afrika 2021

Jengo la Leonardo lina urefu wa mita 22

Historia ya majengo marefu zaidi barani Afrika ilianza mwaka 1973 kufuatia ujenzi wa jumba refu la Carlton Centers mjini Johannesburg , ambalo lilishikilia taji la jumba refu barani Afrika hadi mwezi Aprili 2019 kulingana na mtandao wa CK .

Baada ya kupata sifa ya kuwa na jumba refu zaidi barani , haishangazi kuona kwamba Afrika Kusini imejizatiti kumiliki idadi kubwa ya majumba marefu barani Afrika.

Haya hapa majumba marefu zaidi barani Afrika:

1. Leonardo, Afrika Kusini

Jumba la Leonardo lina urefu wa mita 227-pamoja na ghorofa 56. Jumba hilo lipo katika barabara ya 75 ya Maude, takriban mita 100 kutoka katka jumba la soko la hisa la Johannesburg Stock Exchange.

Kulingana na mtandao wa CK, ujenzi wa jumba hilo ulianza tarehe 17 mwezi Novemba 2015 na liliongoza kwa urefu mwaka 2019 , likishinda rasmi taji la kuwa jumba refu zaidi barani Afrika.

2. Carlton Centre, Afrika Kusini

Jumba la Carlton Center Afrika Kusini

CHANZO CHA PICHA,HOBERMAN COLLECTION

Jumba la Carlton Centre, lenye urefu wa mita 223 ni kituo kikuu cha maduka tofauti – mjini Johannesburg, Africa kusini, limekuwa jumba refu barani Afrika kwa muda mrefu kabla ya ujenzi wa jumba la Leonardo

3. Britam Tower, Kenya

Jumba la Britam Towers

Britam Tower, lina urefu wa mita 200 na limejengwa katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi . Lilifunguliwa rasmi kwa umma 2018 , na kulipiku jumba la UAP Old Mutual kama jumba refu zaidi nchini Kenya.

Jumba hilo lenye ghorofa 31 ambalo lilianza kujengwa mwaka 2013 lilikamilika mwezi Septemba 2017, na linajivunia muundo wa kipekee.

Mwaka 2018, Britam Tower lilikuwa jumba la kwanza barani Afrika kukabidhiwa taji la tuzo la Emporis Skyscraper lenye historia ya miaka 19 baada ya kutajwa kuwa jumba la kumi bora duniani.

Likiwa katika eneo la Upper hill jijini Nairobi jumba hilo lenye ghorofa 31 linatoa mandhari ya kupendeza ambapo unaweza kuona eneo la kati la mji mkuu wa Nairobi pamoja na maeneo ya viungani mwake ikiwemo mbuga ya wanyama pori ya Nairobi.

Ujenzi wake ulikamilika mnamo mwezi Novemba 2017, na sasa linamilikiwa na kampuni ya bima ya Britam Life Assurance Limited.

Katika siku nzuri isio na mawingu unaweza kuona Mlima Kilimanjaro pamoja na Mlima Kenya juu ya jumba hilo.

4. Makao makuu ya CBE, Ethiopia

Jumba hilo lina urefu wa mita 198 na linamilikiwa na benki ya biashara ya Commercial Bank ya Ethiopia (CBE) katikati ya mji mkuu wa Addis Ababa Ethiopia.

Ujenzi wake umemaliza utawala wa jumba la mikutano la muungano wa Afrika AU mjini humo.

Jumba hilo lenye ghorofa 46 ambalo liko karibu na hoteli ya Ras Desta katika barabara ya Damtew lina mita 150,000 mraba likiwa makao makuu ya benki hiyo inayomilikiwa na serikali.

5. Nairobi GTC Office Tower

Majumba ya GTC jijini Nairobi

CHANZO CHA PICHA,PHOTO/COURTESY

Ujenzi wa jumba la Nairobi GTC Office Tower, ambalo ndilo refu kati ya majumba sita ya Global Trade Centre, limeleta mgeni mpya katika orodha ya majumba marefu nchini Kenya.

Jumba hilo lenye urefu wa mita 184 na ghorofa 43 ndilo linalotarajiwa kuwa makao makuu ya kampuni ya China Avic ambayo inataka kujikita katika eneo la Westland mjini Nairobi.

Jumba hilo ambalo ujenzi wake ulianza Julai 2015 liLIkamilika mwezi Disemba 2020.

6. Ponte City, Afrika Kusini

Jumba la Ponte City

CHANZO CHA PICHA,ANADOLU AGENCY

Jumba la Ponte City lenye urefu wa mita 172.8 lipo katika makaazi ya mji wa Johannesburg Afrika Kusini. Likiwa limejengwa 1975, jumba hilo lenye ghorofa 54 limetajwa kuwa jumba la kwanza la mviringo kujengwa Afrika

7. UAP Tower, Kenya

UAP/Old Mutual Towers

Jumba hili lililopo katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi lina urefu wa mita 163 . Liliwahi kuwa jumba refu nchini Kenya na Afrika mashariki kwa jumla lilipofunguliwa mwezi Julai 2016 baada ya ujenzi wake uliochukua zaidi ya miaka mitano.

Awali Jumba la UAP Old Mutual jijini Nairobi ndio lililokuwa likishikilia nafasi ya jumba refu zaidi katika eneo la Afrika ya mashariki likiwa na ghorofa 33

Lilikuwa linafuatiwa katika orodha hiyo na Jumba la Twin Tower mjini Dar es salaam lenye ghorofa 35 na urefu wa mita 153.

8. NECOM House, Nigeria

Kulingana na mtandao wa CK , Jumba la NECOM lililojulikana kama NITEL Tower na awali The NET Building, lina urefu wa mita 158 katikati ya mji wa Lagos .

Ndilo jumba refu rasmi nchini Nigeria na eneo zima la Afrika magharibi. Jumba hilo lililokamilika 1979 ndio makao makuu ya kampuni ya Telecomunication Ltd iliokuwa ikimilikiwa na serikali.

9. Tanzania Ports Authority Tower, Tanzania

Tanzania Ports Authority Tower, Tanzania/facebook

Jumba la Tanzania Ports Authority Tower

CHANZO CHA PICHA,TANZANIA PORTS AUTHORITY TOWER, TANZANIA/FACEBOOK

Jumba la Tanzania Ports Authority Tower, lina urefu wa mita 157 katika mji wa kibiashara wa Dar esa Salaam.

Baada ya ujenzi wake kukamilika 2016, jumba hilo lenye urefu wa mita 40 ndio makao makuu ya halmashauri ya Bandari nchini Tanzania.

10. PSPF Towers, Tanzania

Majumba ya PSPF Towers,

Jengo la PSPF Towers mjini Dar es Salaam nchini Tanzania lina urefu wa mita 153 na linatumika kama ofisi.

Majengo 25 Marefu zaidi duniani

1.Burj Khalifa – Dubai

2.Shanghai Tower – Shanghai

3.Makkah Royal Clock Tower – Saudia

4.Ping An Finance Center – Shenzhen

5.Lotte World Tower – Seoul

6.One World Trade Center – New York

7.Guangzhou CTF Finance Centre – Guangzhou

8.Tianjin CTF Finance Centre – Tianjin

9.CITIC Tower – Beijing

10.TAIPEI 101 – Taipei

11.Shanghai World Financial Center – Shanghai

12.International Commerce Centre – Hong Kong

13.Lakhta Center – St. Petersburg, Urusi

14.Vincom Landmark 81 – Ho Chi Minh City, Vietnam

15.Changsha IFS Tower T1 – Changsha, China

16.Petronas Twin Tower 1 – Kuala Lumpur

17.Petronas Twin Tower 2 – Suzhou, China

18.Suzhou IFS – Suzhou, China

19.Zifeng Tower – Nanjing, China

20.The Exchange 106 – Kuala Lumpur

21.Willis Tower – Chicago

22.KK100 – Shenzhen

23.Guangzhou International Finance Center – Guangzhou, China

24.Wuhan Center Tower – Wuhan, China

25.432 Park Avenue – New York

CHANZOCHA HABARI BBC.