Inahusu “utamaduni wa chinchorro ” ambao, kulingana na uchunguzi wa masalia ya kiakiolojia, jamii hiyo ilitumia njia ya kipekee katika kuitunza miili ya wafu wake,
Zaidi ya miaka elfu 7 iliyopita, eneo tambarare la jangwa la Atacama lilikuwa linakaliwa na kikundi cha wavuvi ambao walitengeneza teknolojia ambayo leo dunia inaitamani .
Inahusu “utamaduni wa chinchorro ” ambao, kulingana na uchunguzi wa masalia ya kiakiolojia, jamii hiyo ilitumia njia ya kipekee katika kuitunza miili ya wafu wake, kwa kutumia mbinu ya ujuzi iliyowezesha miili ya wafu wao kuishi kwa zaidi ya miaka elfu mbili kabla ya Wamisri.
Kazi ya kundi hili ilitambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), ambalo Jumanne wiki hii lilijumisha uhifadhi bandia wa miili wa utamaduni wa Chinchorro kwenye orodha ya urithi ya Dunia.
Kulingana na shirika hilo la kimataifa, utamaduni huu unawakilisha “ushahidi wa kale zaidi wa kiakiolojia wa uhifadhi bandia wa miili ya wafu “, jambo ambalo linaonesha “nafasi ya kimsingi” ya wafu katika jamii hiyo.
Lakini chinchorro walikuwa ni watu gani hasa na ni vipi waliweza kutengeneza mbinu hii ya kushangaza kuifanya miili ya marehemu nduguzao isiharibike?
Kijiji cha uvuvi
Utamaduni wa Chinchorro unapatikana baina ya bandari za Ilo, nchini Peru, na ile ya Antofagasta, upande wa nchi ya Chile.
Licha ya ukame wake mbaya, eneo hili lilikuwa tajiri sana kwa raslimali kutokana na athari za baridi na vijito tofauti vilivyofika kwenye bahari.
Kwa njia hii, jamii ya chinchorros ilijikita katika kutumia raslimali za majini ambapo walitumia vifaa mbali mbali. Miongoni mwa vifaa hivyo ilikuwa ni ndoano iliyotengenezwa na cactus na mkuki wenye ncha.
Kulingana na Unesco, “zana zilizotengenezwa kwa madini na mimea vimepatikana, pamoja na vifaa vilivyotengenezwa kwa mifupa na magamba” ambavyo viliwawezesha “upatikanaji wa raslimali za majini “.
Kulingana na Jumba la makumbusho la nchini Chile ya kabla ya Sanaa ya Columbia , “kutokana na uvimbe uliobainika kwenye masikio ya wafu wa wakati huo, inaaminiwa kuwa walizama katika kina kirefu.”
Kipaji hiki kiliwawezesha kutengeneza eneo ambalo ni sawa na makazi ya kudunu kwenye kingo za mito na vijito kwenye eneo hilo.
Ingawa kuna taarifa chache kuhusu jinsi shughuli hiyo ilivyofanyika, inaaminiwa kwamba walikuwa wanakutana katika makundi makubwa au madogo ya watu kati ya 30 na 50, ya watu wenye uhusiano wa kindugu.
Waliwakaushaje wafu wao?
Kile kinachojitokeza zaidi kuhusu utamaduni huu ni mbinu ngumu walizotumia za kuhifadhi mwili zinazotumiwa katika kuhifadhi maiti, ambazo zinaonesha umuhimu waliopatia ibada ya wafu na mababu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Chuo kikuu cha Tarapacá de Chile, ambacho kimeongoza utafiti na uhifadhi wa utamatuni wa Chinchorro, mchakato huo ulikuwa ni pamoja na kuondolewa kwa viungo vya ndani vya marehemu kwa njia upasuaji na badala yake kuweka mboga, manyoya, vipande vya ngozi, na sufi pamoja na vitu vingine.
PICHA: Hadi sasa miili 208 ya wafu iliyokaushwa imekwisha chunguzwa na mbinu za utunzaji wake zimekuwa zikibainika kulingana na muda
Zaidi ya hayo ilibainika kuwa, ngozi ya kichwa na uso, viliondolewa, na fuvu liliondolewa ili kuondoa ubongo wa marehemu, ambapo eneo hilo la mwili lilipokauka waliingiza majivu, udongo na nywele za wanyama.
Halafu uso ulikarabatiwa, nywele za binadamu zilitengenezwa mfano wa wigi na kuwekwa kwenye kichwa cha marehemu na hatimaye marehemu kuvalishwa vazi la mmea. Mwishowe, mwili ulifunikwa kwa safu za udongo laini.
Ingawa mwanzoni chichorros waliwakausha watoto wanaozaliwa na watoto pekee-na kuwafunika kwa udongo – utamaduni huo ulishamiri zaidi (karibu miaka 3000 BC), wawakilishi wa wajumbe wote wa jamii walihifadhiwa kwa kukaushwa na watu wa rika zote
Aina tofauti za kuwahifadhi wafu kwa kuwakausha
Katika utamaduni wa Chinchorro kulikuwa na wafu weusi, waliopakwa madini ya manganese oxide; wafu wekundu, waliopakwa madini ya iron oxide; na wafu waliohifadhiwa kwa kufungwa vitambaa au bandage.
Wote walikuwa na mambo yanayofanana kama vile kuvalishwa nywele bandia za binadamu, barakoa za uso na vijiti vya kunyoosha miili yao.
” Utamaduni wa Chinchorro uliowaona wafu waliokaushwa kama sehemu ya viumbe wanaoishi duniani, jambo linaloelezea ni kwanini waliyaacha macho na vinywa vyao wazi, na kwamba walitumia machela, zilizotengenezwa kwa nyuzi za mimea na ngozi za wanyama, kuwasafirisha. Wakati mwingine walizikwa kwa pamoja “, Ilielezwa katika Chuo kikuu cha Tarapacá.
Mbinu za kisasa za utunzaji wa maiti, na jangwa pamoja na mazingira ya udongo wa chumvi, viliwezesha kutunzwa kwa miili ya wafu 120 na sasa wamewekwa katika makumbusho ya Kiakioloji ya San Miguel de Azapa, nchini in Chile.
CHANZO CHA HABARI BBC