Mahala unapoishi kwa maana ya makazi ama nyumba panapaswa kuwa salama zaidi kuliko mahali pengine popote.
Ndio sababu ya kukuta nyumba inalindwa na ulinzi wa kila aina kuwezesha usalama wa watu wanaoishi kwenye nyumba husika. Kuanzia madirisha, milango, ukuta mrefu, mageti, waya za umeme, kamera za CCTV na hata kulindwa na walinzi.
Kujilinda kote huku tunafikiria zaidi kuhusu hatari ya kuingiliwa na wanyama, wezi au majambazi na kusahau kwamba kuna hatari nyingine nyingi tunazoishi nazo kila siku bila kujua kwamba ni hatari zaidi kuliko hatari tajwa.
Baadhi ya Vitu vya nyumbani ama vitu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ni hatari na vinaweza kusababisha hata vifo, ukiacha majeraha ama hasara kubwa ya mali.
Viko vingi ila vitu vitano vifuatavyo vya nyumbani hatari zaidi usipokuwa na umakini navyo namna ya kutumia na kuvitunza.
1. Mitungi ya gesi ya kupikia (Gas Cylinder)
Kunao watalamu wa usalama ambao huutaja mtungi wa gesi nyumbani kama ‘bomu linalongoja kulipuka’.Ukitaka kupika kwa haraka, gesi ni nishati nzuri na rahisi kuitumia kuliko mkaa ama kuni.
Watu wa mazingira wanaipigia chapuo hii kwa sababu matumizi yake yanaokoa, athari za ukataji miti hovyo inayotumika kwa kuni na mkaa.
Kwa faida zake, matumizi ya gesi kwa sasa duniani yameongezeka mara mbili zaidi tofauti na karne mbili zilizopita, na matumizi yakionekana kushika kasi zaidi katika nchi za bara la Afrika.
Pamoja na uzuri wa gesi ila ni hatari kama hautozingatia usalama wake. Kwanza gesi inayotumika kupikia inaweza kuwa katika aina tatu tofauti, gesi asili (natural gas), mitungi ya gesi (liquified petroleum gas) na gesi inayotokana na kinyesi (biogas), pamoja na yote, gesi ina tabia ya kuwaka. Kwa mfano gesi ya butane inawaka kwa kasi na haraka zaidi.
Gesi hutoa kaboni yenye sumu na ambayo hushika moto haraka sana, kitendo chochote cha moto wa gesi haipatikani nafasi ya dharura, hufanyika kwa haraka na kwa kasi kubwa kama bomu, hivyo kuleta madhara ya haraka zaidi.
Kwa usalama zaidi, mtungi wako wa gesi ya kupikia uweke nje ya nyumba na tumia mpira wa gesi kupeleka gesi kwenye jiko lenyewe la kupikia.
Watalaam wanasema usitingishe mtungi wa gesi kutambua kama gesi imeisha ama bado, tumia kitambaa kiweke maji kisha paka kwenye huo mtungi kwa pembeni na utaona kiasi kilichobaki.
2: Soketi na nyaya za umeme zilizoacha wazi
Ziko nyaya za umeme zilizowekwa kwenye nyumba kabisa (Wiring) lakini zipo waya za umeme ambazo wengi wanazotumia kwa ajili ya kuunganisha vyombo mbalimbali vya umeme kama kuchaji simu, kompyuta, kupiga pasi na vinginevyo.
Lakini ‘Extension Cable’ hizo ni hatari zaidi kwa muundo, matumizi na panafaa kuwa na tahadhari ya juu wakati zinapotumiwa.Kunazo pia nyaya zinazoachwa wazi ambazo zikiguswa wakati zinapopotisha umeme ,ni hatari saba kwa wanaozitumia .
Nchini Marekani, matukio ya moto yanayosababishwa na ‘Extension Cable’ ndio mengi zaidi kuliko matukio mengine na kuleta madhara makubwa.
3: Polishi za samani
Wamiliki wengi wa nyumba wanapenda kuweka samani (Furniture) ndani kama viti, meza, makabati, stuli na zingine. Samani hizi hupigwa Polishi kung’arishwa ili zipendeze zaidi.
Wapo ambao samani zikitoka kwa fundi zinakuwa zishapigwa tayari polishi na wengine hasa wenye uwezo wanapiga polishi samani zao pamoja na milango na madirisha ya mbao mara kwa mara kwa kutumia polishi za nyumbani kila wanapofanya usafi wa nyumbani.
Anaweza kufanya hivyo mara mbili kwa wiki ama hata kila siku kwa namna anavyoona inafaa lakini Polishi hizi zinatabia ya kuwaka. Zikishika moto, ama zikiwa karibu na moto zinaweza kuleta madhara makubwa.
Mbali na kuwaka moto, Polishi zinazotumika kung’arisha samani zina kemikali aina ya phenol na nitrobenzene, ambazo zikinyonywa na ngozi yako zinaweza kusababisha saratani ya ngozi.
4: Sabuni za kupambana na bakteria
Sabuni za za kukambana na bakteria (Antibacterial Soaps) nyingi ni za kuogea. Zinatajwa kuwa ni sabuni nzuri kwa ajili ya kukabiliana bakteria na wadudu wengine wanaosababisha magonjwa mbalimbali.
Lakini katika hizi sabuni kuna vitu vinawekwa kusaidia kufanya kazi kwake vizuri dhidi ya bakteria, vinaitwa triclosoan na triclorcarbon ambavyo vinaleta madhara kwa binadamu.
Licha ya mamlaka kuziruhusu kutokana na kupima faida yake kubwa dhidi ya hasara za aina hizi za sabanui, bado hasara hizo ndogo zinaweza kuwa kubwa kwa mtu mmoja mmoja kwa uchache.
Moja ya hasara yake inaelezwa triclosoan na triclorcarbon zinaweza kutengeneza vijidudu sugu vinavyoweza kuleta magonjwa kwa mtumiaji.
5: Sabuni za chooni
Ukiacha choo chenyewe ambacho kinaweza kuhifadhi wadudu na kukudhuru, Kwa watu wenye vyoo vya kisasa na bora, hutumia zaidi sabuni maalumu (Toilet Bowl Cleaner) kusafishia vyoo vyao, sabuni hizi nyingi ni za maji zikihifadhiwa kwenye madumu yenye ujazo tofauti, kuanzia lita moja mpaka lita ishirini.
Kama zilivyo sabuni za kukabiliana na bakteria, sabuni za kusabifisha choo pia ziwekewa vichocheo ‘corrosive ingredients’ ambavyo vinafanya sabuni hizo zifanye kazi vizuri zaidi. Lakini vitu hivyo vinaweza kusababisha pia kuharibu ngozi yako na hata macho. Ni hatari zaidi zikichanganywa na sabuni zingine za aina hiyo, ama kimiminika chenye kemikali zinazokabilina na bakteria.
Muhimu tumia vikinga mkono (gloves) wakai wote unapozitumia kusafisha choo chako ama kuzihaisha kutoka sehmu moja kwenda nyingine.
CHANZO CHA HABARI BBC