Wednesday, January 15

YANGA YATOKA SARE YA PILI MICHUANO YA KAGAME CUP 2021

Timu ya Yanga imeshindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Atlabara kutoka Sudan Kusini baada ya sare ya bila kufungana katika mwendelezo wa  mechi za Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Huu ni mchezo wa pili wa Yanga kupata sare baada ya mchezo wa ufunguzi dhidi ya Nyasa Big Bullet ya Malawi  kutoka sare ya 1-1.

Kwa Mchezo huo Yanga wamefikisha Pointi mbili Michuano hiyo itaendelea kesho katika uwanja wa Chamazi Complex nje kidogo ya Dar