Wednesday, January 15

Afya yashinda bao 2-1 dhidi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndenge Pemba.

NA ABDI SULEIMAN.

TIMU ya Wizara ya Afya imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya timu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndenge Pemba, ikiwa ni mwendelezo wa robo fainali ya mashindano ya Wizara Cup.

Mashndano hayo yaliyojumuisha timu mbali mbali za wizara ya Serikali Pemba, na kuvuta hizisia za mashabiki wa soka kisiwani hapa.

ZAA ilikuwa ya kwanza kupata bao lake katika dakika ya 20 uwanjani hapo kupitia kwa mchezaji Said Hassan, balo lililodumu hadi timu zinakwenda mapumziko.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi huku Afya wakitaka kusawazisha na ZAA kuongeza bao, bahati iliwangukia Afya iliyoweza kusazisha goli na kuongeza jengine.

Bao hilo la Wizara ya Afya lilipachikwa wavuni na mchezaji Mohamed Salim Mohamed, hadi mchezo unamalizika Wizara ya Afya bao 2-1 dhidi ya ZAA.

Kwa matokero hayo timu ya ZAA imeungana na Wizara ya Utalii na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi.