NA MWANDISHI WETU.
TIMU ya Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Pemba, imewasilisha malalamiko yao kwa kamati ya mashindano ya Wizara Pemba, juu ya timu ya Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Pemba kuwachezesha wacheza watatu kinyume na kanuni za mashindano hayo.
Kwa mujibu wa barua kutoka kwa mratibu wa michezo Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Pemba, kwenda kwa katibu wa kamati ya Mashindano ya Wizara, ya Agosti nane mwaka hu, imewalalamikia wachezaji Suleiman Juma Bakari jezi namba 10, Abass Moh’d Faki jezi namba 30 na Moh’d Mzee Moh’d jezi namba 7 pamoja na watumishi wa wizara hiyo .
Barua hiyo imesema Mchezaji Suleiman Juma Bakar alifungiwa na kamati hiyo, kutokushiriki michezo hiyo kwa barua rasmi iliyotolewa na kamati lakini hadi mchezo wa Agosti 4 unachezwa hakuna barua ya majibu kutoka kwa kamati kwenda Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi kuwa mchezaji huyo maruhusiwa kuchezwa.
Aidha barua hiyo imeendelea kueleza kuwa mchezaji Abass Moh’d Faki na Moh’d Mzee Moh’d kwa pamoja hawamo katika fomu ya usajili ulio wasilishwa awali na kuonekana katika usajili feki.
Barua hiyo imeenda mbali zaidi na kudai kuwa, upande wa nidhamu mfanyakazi wa wizara ya Ujenzi alimpiga rifarii teke muda wa mapumziko na hakuna adhabu yopyote iliotolewa kwa wenginbe isirejee, kitendo kilichotoa mshtuko wa kukosa amani na usalama michezoni.
Hata hivyo malalamiko mengine ni kwamba timu ya Wizara ya Ujenzi haikuweza kushiriki mchezo wa mwanzo bila ya sababu maalumu na kamati hyako iliweza kutoa barua ya kuwataka kulipa faini ambapo faini hiyo haijalipwa huku mashindano yakielekea ukingoni.
“Mambo haya yanatupelekea sisi na timu zengine zilizoshiriki michezo haya kuona hakuna uadilifu na ubora wa mashindano kwani matendo yake sio ya kiutumishi wa serikali”ilisema baraua hiyo.
Hata hivyo iliitaka kamati hiyo kuyachukuliwa kwa uzito mkubwa mambo hayo, ili kulinda hadhi ya mashindano, nakala ya barua hiyo imetumwa kwa waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na michezo, katibu Mkuu Wizara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ofisa Mdhamini Wizara habari Vijana Uatamaduni na Michezo Pemba na katibu wa michezo wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi