NA SAID ABRAHMAN.
MASHINDANO ya elimu bila malipo ngazi ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, yaliendelea tena katika Kiwanja Cha Kinyasini Wete kwa upande wa michezo ya riadha.
Michezo hiyo ambayo iliweza kushindaniwa ni pamoja na mbio mita 100,1500,2000,3000,5000 relaya kubwa na ndogo ( Mbio za kupokezana vijiti), ambapo Skuli zote ambazo ziliweza kufanya vizuri katika Wilaya zao ziliweza kushiriki.
Kwa upande mbio mita 100 kwa Skuli za Sekondari wanawake mshindi alikuwa ni Hadia Mbwana Hamad ( Kiuyu), Sijaona Mkwapi Makenzi, (Gando) na Zakia Ahmad Hamad (Shumba)
Kwa upande wa mita 800, mshindi ni Fatma Rashid Mbarouk (Gando) Moza Said Mussa (Kiuyu) na Naifat Rashid Salim ( Dk, Shein).Mita 200 mshindi ni Sharifa Salim Hamad (Kiuyu), Sijaona Mkwapi Makenzi (Gando), na Salma Juma Iddi (Gando).
Ama kwa upande wa mita 1500, washindi ni Time Suleiman Mussa (Mchangamdogo),Siti Abdalla Said (Shumba), na Naifat Abbas Kombo (Gando).Kwa upande wa Mbio mita 400 washindi ni Fadhila Mbarouk Khamis (Tumbe), Zainab Salim Abdalla (Kiuyu) na Samira Massoud Mohammed (Tumbe).
Mita 3000, washindi ni Asha Mussa Rashid (Gando), Fatma Rashid Mbarouk (Gando) na Fatma Mbarouk Mohammed (Gando). Kwa upande wa ‘ relay kubwa’ washindi ni Salma Sharif Hamad (Kiuyu), Salma Juma Iddi (Gando) na Sada Salim (Tumbe) huku ‘relay ndogo washindi ni Raya Shibu Sharif (Gando), Riziki Faki Hamad (Kiuyu) na Rehema Mussa (Tumbe).
Kwa upande wa urushaji wa tufe, washindi ni Bimkubwa Bakar Suleiman (Kiuyu), Sada Salim (Tumbe) na Salma Mjaka Salim (Tumbe) huku Kamba washindi ni Micheweni na Chwaka. Kwa upande wa urushaji mkuki washindi ni Salama Khamis (Tumbe), Bimkubwa Bakar Suleiman (Kiuyu) na Maryam Bakar Omar (Tumbe).
Kwa upande wa wanaume Sekondari mita 100, washindi ni Faki Hamad Faki (Kiuyu),Amour Abdalla Mbarouk (Pandani) na Riadh Amour Mohammed (Gando) huku mita 800 washindi ni Hamad Ali Omar na Khamis Omar Hamad (Gando).
Mita 200, washindi ni Khamis Faki Khamis (Tumbe), Said Haji Ame (Gando) na Abdulsalaam Kombo Salim (CCK) huku mita 1500 washindi ni Abdalla Ame Kombo (Gando), Nassor Hussein Faki (Mchangamdogo) na Said Haji Ame (Gando).
Kwa upande wa mita 400,washindi ni Mohammed Khamis (Tumbe), Ali Massoud Said (Shumba) na Juma Omar Ali (CCK) huku mita 3000 washindi ni Abdalla Shineni Khamis (Dk, Shein), Khamis Ali Hassan (Micheweni) na Suleiman Ali Khamis (Gando).
Kwa upande wa Mbio za kupokezana vijiti, (relay kubwa) washindi ni Mohammed Khamis (Tumbe), Pazi Amour Mohammed (Gando) na Hamad Khamis (Kiuyu) huku ‘relay ndogo washindi ni Riadh Amour (Gando), Said Muhammed (Tumbe) na Ali Mohammed (Shumba).
Ama kwa upanda wa urushaji wa mkuki, washindi ni Said Kombo Ali (Tumbe), Amour Abdalla Mbarouk (Shumba) na Seif Khamis Omar (GTumbe) huku washindi wa urushaji kisahani ni Seif Khamis Omar (Tumbe) na Amour Abdalla Omar (Shumba).
Kwa upande wa msingi wanawake mita 100, washindi ni Saumu Kombo Suleiman (Shumba),Zainab Shaib Yahya (Shumba) na Zainab Khamis (Tumbe) huku wanaume washindi ni Ibrahim Juma Omar (Wingwi), Nassor Khalfan Juma (Tumbe) na Miraji Khamis Suleiman (Mchangamdogo)
Ama kwa upande wa mita 800 wanawake washindi ni Saumu Omar Ali (Gando), Rehema Khamis (Mchangamdogo) na Asha Kassim (Shumba vyamboni) huku wanaume ni Salim Omar Ali (Wingwi),Khatib Shoka Faki (Maziwang’ombe) na Omar Salim Ali (Tumbe).
Kwa upande wa mita 200, wanawake washindi ni Salma Omar Ali (Gando),Hadia Juma Faki (Maziwang’ombe) na Saumu Salim Ali (Shumba vyamboni) huku wanaume washindi ni Hamad Juma Bakar (Tumbe), Kombo Simba Faki (Maziwang’ombe) na Khamis Mohammed Salim (Mabarini).
Mita 1500 wanawake washindi ni Wanu Khamis Yahya (Karume), Ramla Ali Juma (Tumbe) na Asha Omar Faki (Wingwi) huku wanaume washindi ni Ali Rashid Ali (Wingwi) Massoud Khalfan Mohammed (Mabatini) na Yussuf Ali Rashid (Gando).
Mita 400 wanawake washindi ni Sada Omar Ali (Gando), Amina Iddi Hamad (Tumbe) na Fatma Haroun Juma (Tumbe) huku wanaume washindi ni Khatib Shoka Faki (Maziwang’ombe), Faki Salim Juma (Shumba) na Nassor Khalfan Juma (Tumbe).
Kwa upande wa ‘relay kubwa, washindi ni Salma Salim Ali (Karume), Eliza Mkwabi Makenzi (Gando) na Maimuna Suleiman (Mabatini) huku wanaume ni Suleiman Ali Salim (Tumbe), Twalhata Hadaa Hamad (Karume) na Sharif Hamad Iddi (Gando).
‘Relay ndogo wanawake washindi ni Maryam Rashid Bakar (Gando), Sada Bakar Omar (Karume) na Najma Abeid Massoud (Shumba) huku wanaume ni Omar Hamad Omar (Tumbe), Twalhata Hadaa Hamad (Kiuyu) na Omar Salim Ali (Shumba vyamboni).
Kwa upande urushaji mkuki washindi wanawake ni Samira Ali Faki (Wingwi), Asha Mohammed Ali (Karume) huku wanaume ni Ali Hamad Khamis (Tumbe), Sharif Juma Mwalimu (Wingwi) na Miraji Hamad Burhan (Mchangamdogo).
Ama kwa upande wa urushaji kisahani washindi kwa wanawake ni Fatma Najim Hamad (Chwale), Maryam Ali Hamad (Wingwi) na Salma Mohammed Ame (Chwale) huku wanaume ni Twalhata Hadaa Hamad (Karume) na Ilyasa Omar Mbwana (Chwale).
Kwa upande wa urushaji tufe, washindi wanawake ni Halima Hamad Juma (Chwale), Siti Haji Bakar (Karume) na Salma Habib Juma (Wingwi) huku wanaume ni Ali Mohammed Khamis (Wingwi) na Ali Hamad Khamis (Tumbe).
Mashindano hayo yanatarajiwa kuendelea tena mwishoni mwa wiki hii kwa upande wa sanaa huko katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Mchangamdogo Wilaya ya Wete.