Sunday, November 24

Mashindano ya vikundi vya sanaa yafanyika uwanja wa michezo Gombani

WASANII wa Ngoma ya Kirumbizi kutoka Pujini Salum Shaame Othman na Mohamed Juma Omar, wakicheza ngomba hiyo kwa kupigana fimbo wakati wa mashinano ya Vikundi vya Sanaa, mashindano yaliyofanyika Gombani Chake Chake Pemba
WASANII wa Ngoma ya Msewe Juma Ali Juma na Khamis Hamad Ali kutokma kambini kichokochwe, wakionyesha umahiri wakucheza ngoma hiyo wakati wa mashindano ya vikundi vya sanaa, mashindano hayo yaliyofanyika Gombani Chake Chake Pemba
MSANII Time Kai Hamad kutoka kikundi cha Uringe kutoka Micheweni akiwaongoza wenzake katika kucheza ngoma ya uringe, wakati wa mashindano ya Vikundi vya sanaa mashindano hayo yaliofanyika Gombani Chake Chake Pemba
WASANII wa Ngoma ya Mkota Ngoma kutoka Mkoani, wakionyesha burudani ya ngoma hiyo katika mashindano ya Vikundi vya sanaa mashindano hayo yaliyofanyika Gombani Chake Chake Pemba
KATIBU Mkuu wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatama Hamad Rajab, akizungumza wakati wa mashindano ya Vikundi vya Sanaa mashindano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba
WAZIRI wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulidi Mwita, akizungumza na wasanii mbali mbali wakati wa mashindano ya vikundi vya sanaa mashindano yaliyofanyika katika uwanja wa michezo Gombani

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

NA ABDI SULEIMAN.

WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulidi Mwita, amewataka wasanii wa vikundi vya sanaa Ksiiwani Pemba, kuhakikisha sanaa hiyo wanawarithisha vijana wao ili iweze kuendelea kudumu.

Alisema sanaa nyingi zimekua zikipotea kutokana na wazee kushindwa kuzirithisha kwa vijana wao, jambo ambalo linapelekea sanaa hizo kupotea siku hadi siku.

Waziri Tabia aliyaeleza hayo katika hutuba yake wakati wa mashindano ya vikundi vya sanaa Pemba, yaliyofanyika uwanja wa Michezo Gombani Chake Chake Pemba.

Aidha alisema Wizara itahakikisha inakamilisha yale yote yanayohitajika katika kuboresha sana za utamaduni zikiwemo ngoma za asili, ili ziweze kuendelea kubaki katika asili yake na kurisishwa kwa vizazi vya sasa vilivyopo bila ya kupoteza asilia yake.

“Tayari sisi kama Wizara tumeshaanza kuchukua hatua za kuviboresha vikundi mbali mbali vya sana, kwa kuanda matamasha na mashindano na matamasha mbali mbali ya asili”alisema.

Hata hivyo alisema wizara itaendelea kuimarisha kitengo cha haki miliki, ili wasanii waweze kupata haki zao wale ambao wataweza kuzisajili sanaa zao.

Naye Katibu mkuu wa wizara ya habari utamaduni na michezo Fatama Hamad Rajab, alisema Wizara imejipanga kuleta mabadiliko makubwa katika sana, hivyo aliwataka wasani kutoa mashirikiano yao ili kufanikisha malengo ya wizara ya kuboresha sana.

Kwa upande wake Mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo Ibrahim Bukenga, ameitaka wizara kuhakikisha inawasimamia wasanii katika kulinda utamaduni wa mzanzibari amboa ndio urithi wa Zanzibar.

“Sanaa inapotumika katika majukwaa mbali mbali inatoa alama kubwa kwa taifa nan chi, hivyo ipo haja wasanii wetu kuendelea kuutangaza utamaduni wa mzanzibar na kutokuharibu”alisema.

Akitoa neno la shukurani kwa niamba ya vikundi vya sana Msanii Mohammed Kombo(mwenyi mpeku) aliutaka uongozi wa wizara, kukaa pamoja na vikundi vya sana kisiwani Pemba, ili kushirikiana katika kuboresha sana ikiwemo ya ngoma za utamaduni na sana za maonyesho.