Thursday, January 16

Utalii yaipiga Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba bao 3-0 .

OFISA Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba Zuhura Mgeni wa kwanza kushoto, akizungumza na kepteni wa timu yake Mussa Said, wakati wa mapumziko ili kuwatia hamasha wachezaji wake na hatimae timu yake ikaibuka na ushindi wa Bao 3-0 dhidi ya Timu ya Ofisi ya Rais Katiba sheria Utamishi na Utawala Bora, mchezo uliochezwa Gombani.     (PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

NA ABDI SULEIMAN.

TIMU ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, imefanikiwa kuwafundisha masuala ya utalii kwa wate, timu ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba baada ya kuikunuta kwa bao 3-0 katika mashindano ya mawizara.

Mashindano hayo yanayoendelea kurindima katika uwanja wa michezo Gombani, nakuvuta hamasa kwa mashabiki wa timu hizo, zikiungwa mkono na maafisa wadhamini wa wizara zao.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa michezo Gombani majira ya saa kumi za Jioni, huku kila timu ikicheza kwa tahadhari kubwa katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Wizara ya Utalii ilianza kuzifumania nyavu za Wizara ya Katiba dakika ya 20 kupitia kwa Ali Ussi, bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamazilika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikiwa imepata mawaidha ya walimu wao, huku Wizara ya Utalii ikiongozwa na kutiwa hamasha na Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo.

Ilichukua dakika 64 tu kwa utalii kuandika bao la pili, lililofungwa kwa mkwaju wa penant kupitia kwa Issa Abass, huku Ali Ussi kwa mara ya pili akipachika bao la tatu dakika ya 77 na kuvunja ndoto za Wizara ya katiba sheria kusonga mbele kwenye hatua ya Nusu Fainali ya mashindano hayo.

Kepteni wa Wizara ya Utalii Mussa Said, alisema kwao kila mchezo ni fainali kwani watahakikisha ubingwa wa mashindano hayo unabakia mikononi mwao.

Naye kiongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba sheria Mohamed Suleiman, alisema mchezo haukuwa wao kwani walijitahidi kutafuga bao lakini wakaambulia kupoteza.

Mchezo wa kwanza war obo fainali timu ya Wizara ya Nachi Ofisi ya Rais Fedha ilikubalia kipigo cha bao 3-2 dhidi ya Timu ya Wizara ya Ujenzi.