Thursday, January 16

Waandishi watakiwa kutumia taaluma yao juu na kuifunza jamii elimu ya uraia ili wafahamu haki na wajibu wao.

NA KHADIJA KOMBO- PEMBA.             

Kukosekana  kwa uwelewa mzuri   juu ya  elimu ya uraiya ndiko kunakosababisha wananchi kushindwa kufahamu namna ya kudai haki zao za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba  katika mafunzo ya kuwajenga uwezo wanawake waweze kudai haki zao kiuchumi kisiasa na kijamii huko katika Ukumbi wa Ofisi za TAMWA Pemba Muhadhiri kutoka Chuo Kikuu Zanzibar ( SUZA) Dr. Mzee  Mustafa Mzee amesema wananchi wana haki ya kudai haki zao kila wanapo baini kwamba zimekosekana lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa  kutokufahamu haki na wajibu wao   kunakosababishwa na kutoitambua vyema    elimu ya uraiya .

Dr. Mzee Amesema  kutokana na uwezo wa vyombo vya habari  kuandika pamoja na kuandaa vipindi mbali mbali wanaweza kujikita zaidi katika kutoa taaluma juu ya elimu ya kiraiya ili kila mmoja akaweza kufahamu haki na wajibu wake  ndani ya jamii.

Akizungumzia kuhusu ushiriki wa wananchi katika kupanga maendeleo endelevu amesema kila mtu anahaki ya kutoa ushiriki wake hasa katika kuibua changamoto zinazo wakabili ili kupanga mikakati ya pamoja katika kutatua changamoto hizo na kuleta mabadiliko ya maendeleo lakini watu wanashindwa kutoa ushiriki wao kutokana na kutofahamu  wajibu na haki hizo.

Akielezea kuhusu lengo la mradi huo amesema ni kuwawezesha waandishi wa habari  kuandika habari za uchambuzi  zitakazo saidia wananchi  hasa wanawake  kutambua namna ya kudai haki zao pale mbapo zimekosekana kutoka na  baadhi ya viongozi kutokuwajibika ipasavyo.

Kwa upande wao waandishi hao wamesema watahakikisha mafunzo hayo wanayafanyia kazi ili jamii hasa wanawake  waweze kupata uwelewa na kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa mafufaa ya wananchi wote.

Mradi wa kuwajenga uwezo wanawake  waweze kudai haki zao kiuchumi kisiasa na kijamii unaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TAMWA Zanzibar , Jumuiya ya wanashiria wanawake  ZAFELA, pamoja na PEGAO  umekuwa ukitoa mafunzo kwa watu katika makundi mbali mbali ikiwemo waandishi wa habari.